Kaimu Mkurugenzi wa TMA, Dk. Ladialaus Chang’a akifungua semina hiyo.
Baadhi ya wanahabari wakisikiliza hotuba.
Kibaha, Tanzania
BAADHI ya Waandishi wa Habari kutoka jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye semina ya siku moja leo Septemba 1.2021 katika Chuo cha Uuguzi mjini Kibaha Mkoa wa Pwani, iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), kuhusu mwelekeo wa utabiri wa mvua za msimu wa Vuli zitakazoanza Octoba hadi Desemba mwaka huu.
Katika semina hiyo iliyofunguliwa na Kaimu Mkurugenzi wa TMA, Dk. Ladislaus Chang’a wanahabari hao walielezwa na kushiriki kuvijadili viashiria mbalimbali vinavyotumika kukusanya taarifa sahihi kwaajili ya tabiri mbalimbali ikiwemo ya vuli.
Semina hiyo ni miendelezo wa semina za kila mwaka zinazoshirikisha wadau wa TMA kabla ya kutangzwa kwa utabiri wa msimu husika. Hivyo wadau hao wanapata mrejesho wa utabiri uliotangulia na mwelekeo wa utabiri ujao.
Akifungua semina hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi, Dk. Chang’a aliwapongeza wanahabari kwa kuongeza wigo wa ufahamu wa taarifa za utabiri kwa jamii na kuwataka kuendelea kuandika taarifa sahihi za hali ya hewa mara kwa mara badala ya kusubiri msimu hadi msimu.
No comments:
Post a Comment