September 25, 2021

DAR NI NYEKUNDU AMA NJANO/ NYEUPE AMA KIJANI?


Na John Marwa


Àsikwambie mtu Leo hapatoshi Estadio De Benjamin Mkapa 'LUPASO' Miamba isiyoshindika inaposhuka Dimbani kukata utepe wa msimu mpya wa kabumbu Tanzania Bara TPL 2021/2022.

Ni Simba Mnyama wa mwitu Bingwa wa Soka Tanzania misimu minne iliyopita akishuka nyasini kusakata gozi la Ng'ombe na Wananchi Dar es Salaam Young Africans.

Ni Vita ya Nyekundu kwa Njano, Nyeupe kwa kijani. Mchezo wa Ngao ya Jamii utakaohitaji mmoja kucheka leo pale Lupaso bila hiyana lazima wakulia walei wa kucheka wacheke na watacheka Sanaa na kulia sanaaa Leo.

Mchezo huu kama ilivyo michezo mingine ya watani wa Jadi mzuka wake sio wa kitoto ni ubabe tu, Juhudi za asilimia zaidi ya 💯 na fundi wa wakufunzi ukimaliza mchezo ama kuulaza mchezo... Hali mtu Leo.

Ukikitizama kikosi cha Simba kina uwanda mpana wa kuzilizisha nyoyo za wana Msimbazi ambao bado mashaka yuko mioyoni mwao bado Chama ni Miquissone wanadunda kwenye mapigo ya Mioyo yao ni kazi ya Gomes na wasaidiizi wake kuwafanya akina Sakho, Banda na Kounoute kuwa kitubio kwa wapinzani.

Kwa Wananchi nako mambo ni bull nongwa, kikosi kiko na vipaji jadidi lakini mtori na nyama urafiki uko chini.

Swali ni je Professor Nabi atawadumbukiza Aucho, Djuma na Mayele kuwa nyama ndani ya mtori? Kila mwana Yanga anatamani kuliona Hilo basi dakika 90 zitasema nao.

Mchezo wa leo ukiamuliwa kimbinu kwa ushidni na Kwa kupoteza basi ni wazi wali umeiva walaji wajiandae kuanzia September 27.
Leo natizama uwezo Binafsi ukiamua mchezo kwa pande zote mbili timu work ikiondoka na taji.

Football game is the game of calculation theory. Mchezo wa Soka umebebwa na dhana ya kimahesabu ndio hapa, Chemistry, Physics na Mathematics zinaingia lakini Matrix Equation, Logarithm Theory na Probability actions zinaaamua mchezo.

Ila Leo Probability actions ndizo zitaamua nani aondoke na mwali sio Matrix Equation wala Logarithm Theory.

Tunaposema probability action ni namna wachezaji wataamua kuuchukua mchezo na kuuweka mabegani mwao, kutaka Kila sekunde, kulazimisha kila tukio na kufanya kila nafasi kuwa dhahabu Uwanjani. Ni kuona naweza kufanya na kufanya zaidi naweza kushinda na kushinda kimatendo.

Leo kamati za ufundi zitapumzika kuacha mpira ujiamue wenyewe. Kila la heri kwa Klabu zote mbili, hongera kwa atakaye Cheka na polee kwa atakayetoka kichwa chini.

Vidole vya DHAHABU John Richard Marwa.

No comments:

Post a Comment

Pages