September 21, 2021

Kampeni ya changia damu kuokoa maisha yanoga

 

Dk.  Avelina Mgasa Mkuu wa Idara ya Ukusanyaji Damu katika Mpango wa Taifa wa Damu Salama.

Dk. Avelina Mgasa akielezea namna damu salama inavyotuzwa baada ya kupimwa.
Dk. Pendaeli Joseph Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Mpango wa Damu Salama.


Na Mwandishi Wetu

 

Mpango wa Taifa wa Damu Salama nchini umezindua kampeni ya kitaifa ya kuihamasisha jamii kuchangia damu ili kuokoa vifo kwa wajazito vinavyotokana na uzazi.


Takwimu za vifo vya uzazi za Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee zilizokusanywa kutoka Januari hadi Desemba mwaka 2020 zinaonyesha asilimia 26.3 ya vifo vingi vilisababishwa na kutokana na kutoka damu nyingi baada ya kujifungua.


Akizungumzia Kampeni hiyo, Mkuu wa Idara ya Ukusanyaji Damu katika Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Dk. Avelina Mgasa amesema kauli mbiu ya kampeni za mwaka huu ni Changia Damu Kuokoa Wanaoleta Uhai Duniani.


Kampeni hii inalenga kuihamasisha jamii kujitolea kutoa damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya kina mams wajawazito ambao wanatumika kama chombo cha kuleta uhai duniani, anasema Dk. Mgasa na kuongeza;


Kauli mbiu inatupa hamasa na kuihamasisha jamii kujitolea kuchangia damu kwa hiari ili kuongeza upatikanaji wa damu ya kutosha na salama ambayo itasaidia kuokoa maisha ya kina mama ambo hupoteza maisha kila siku kutokana na matatizo ya uzazi na wakati wa kujifungua.


Kampeni hiyo iliyozinduliwa katika Kanda zote saba za kukusanya damu nchini zimeanza Jumatatu (jana) Septemba 20 imelenga kukusanya chupa za damu 19,514 kutoka kwenye timu 226 zilizopo nchi nzima ambazo ni asilimia tatu ya malengo yao ya damu kwa mwaka.


Dk. Mgasa amesema kampeni ya mwaka huu inailenga jamii kuwa wachangiaji wa damu kwani asilimia 80 ya damu inayokusanywa nchini inakusanywa kutoka kwa wanafunzi na vijana wanapokuwa shule za sekondari na vyuoni.

No comments:

Post a Comment

Pages