September 22, 2021

TAARIFA YA MKUTANO WA MWAKA WA MASHIRIKA YA KISERIKALI


 Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Uratibu Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini (NaCONGO) imeandaa Mkutano wa  Mwaka wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuanzia tarehe 29-30 Septemba, 2021. 

Mkutano huu utafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma ukiwa na kauli mbiu isemayo: "Kuimarisha Mchango wa Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali katika Maendeleo ya Taifa". 

Mgeni Rasmi katika Mkutano huu ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanaalikwa kushiriki Mkutano huu kwa kujiandikisha kupitia tovuti ya www.nacongo.or.tz au piga namba +255 689 489554  au 0737569583 na 0737569584 kuthibitisha ushiriki wako. 

Ujumbe huu umetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) kwa ufadhili wa Shirika la Legal Services Facility.

No comments:

Post a Comment

Pages