September 26, 2021

KESI YA 'MAMA LEILA' NA WENZAKE MAHAKAMA KUU KUTOA HUKUMU OKTOBA 29


MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imepanga kutoa hukumu ya wafanyabiashara tisa akiwamo Mwanaidi Mfungo (59), maarufu kama Mama Leila  wanaokabiliwa na mashtaka ya kuingiza nchini dawa za kulevya aina ya heroine na cocaine kilo tano.


Hatua hiyo imefikiwa baada ya Jamhuri kuita mashahidi wanane na kuwasilisha vielelezo 21 dhidi ya washtakiwa na utetezi kuita mashahidi tisa.

Kesi hiyo imesikilizwa mbele ya Jaji Isaya Arufani na mawakili wa pande zote mbili kuwasilisha hoja za majumuisho ya mwisho, Jamhuri wakiomba mahakama iwaone wana hatia na utetezi wakiomba mahakama iwaone hawana hatia na  iwaachie huru.

Jaji Arufani alisema baada ya kusikiliza ushahidi na majumuisho ya mwisho mahakama yake itatoa hukumu Oktoba 29, mwaka huu.

 
Mbali na Mfungo washtakiwa wengine ni,Sara munuo (47) Anthony Karanja (42), Ben Ngare (36), Almas Said, Yahaya Ibrahim, Aisha Kungwi na Rajabu Mzombe ambao walisomewa Mashtaka yao kwa mara ya kwanza 2011 mpaka sasa ni miaka 10, wako mahabusu.


Katika kesi ya msingi, ilidaiwa  kuwa, Juni Mosi, 2011, eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, washtakiwa walikamatwa wakiingiza dawa za kulevya aina ya Cocaine.

Washtakiwa walikana mashtaka hayo.

No comments:

Post a Comment

Pages