September 04, 2021

MAKAMU NA WATAALAM WA ARDHI- VERDE

Mkurugenzi wa Jumuiya waliopata nafuu Abdulrahman Abdalla Mani akipokea cheti cha kumaliza mafunzo.


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, amesema serikali imedhamiria kuleta mageuzi katika maendeleo ya makaazi, biashara na uendelezaji ardhi ili kiwe kichocheo cha ukuaji wa uchumi  Zanzibar.

Othman aliyasema hayo janalipofungua kongamano na mkutano wa pili wa Taasisi ya wataalam wa Milki Kuu Tanzania huko katika hoteli ya Verde Mtoni  mjini Zanzibar.

Hata hivyo, Mhe. Othman amesema kwamba migogoro ya ardhi iliyopo bado ni kitendawili na ni tatizo kubwa linalohitaji juhudi za makusudi kupatiwa ufumbuzi wa haraka na kwamba wataalamu wanaweza kuwa na mchango mkubwa katika kupatikana suluhisho  sahihi la tatizo hilo.

Alisema kongamano hilo linalowakutanisha wataalamu mbali mbali wa masuala ya ardhi, uwekezaji , wathamini wa majengo na Maafisa ardhi  litasaidia kujadili na kutafuta  njia muafaka  za matatizo ya ardhi ili kuifikiasha Tanzania katika uchumi bora kupitia tasnia hiyo.

Aliongeza kwamba iwapo suluhisho la migogoro ya ardhi litapatikana  wananchi watatekeleza ipasavyo majukumu yao ya kilimo , ufugaji na ujenzi kwa tija zaidi kuliko ilivyo sasa.

Alifahamisha kwamba hivi karibuni serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefanya mabadiliko katika sheria ya Kukuza na Kuendeleza Uwekezaji Zanzibar, ambayo yanalenga kufungua furasa zaidi za uwekezaji  kwa upande wa kisiwa cha Pemba kwa nia ya kukuza uchumi na maeneleo ya Zanzibar.

Makamu aliongeza  kwamba mabadiliko hayo ya kisheria pia yamelenga kuongeza fursa na vivutio  vipya vya  uwekezaji  wa biashara ya majengo  pamoja na wanunuzi wa nyumba zilizoko katika miradi ya uwekezaji Unguja na Pemba.

Aliwakumbusha wataalamu wa mipango miji kuelewa kwamba nchi imevurugika sana kwenye eneo hilo, kwani ipo mitaa mingi ambapo maumbile yake yengekuwa ya kuvutioa sana  na yenye haiba na thamani kubwa lakini kukosekana ama kutosimamiwa mipango miji  ipasavyo  imefanya miataa hiyo kuwa duni na isiyo na thamani.
 
‘Ninaamini mipango miji na usimamizi wake ni moja   ya mambo muhimu sana  katika kubadili,  sio tu haiba bali pia thamani  ya ardhi na Majengo. Miapngo miji na bora na usimamizi  wenye ufanisi ungefanya mabaraza yetu ya miji kuwa na mapato ya kutosha  kutekeleza kazi zao” alisisitiza Makamu.
Alisema yapo maeneo mengi ambayo thamani ya majengo yaliyopo hayafani kabisa na thamani ya aridhi unaoweza kukadiriwa kwa uhalisia wake.

Naye Rais wa Taasisi ya wataalam wa Milki Kuu  Tanzania ndugu. Andru Katto alisema kwamba Tanzania inashuudia ongezeko kubwa la biashara ya majengo ambapo usimamizi wake husimamiwa na watu wasiokuwa wataalamu wa sekta hiyo.

Alisema jambo hilo nikinyume na nchi nyingi ambapo uuzwaji wa nyumba hufanywa na mawakala  waliosomea na kujisajili chini ya sheria maalum zinazokuwepo.

Alitoa wito kwa wataalamu na washiriki wa kongamano hilo kushirikiana na serikali katika kuyatafutia fumbuzi matatizo ya ardhi ikiwa ni pamoja na serikali kuanzaia sheria inakayodhibiti usimamizi holela.

No comments:

Post a Comment

Pages