September 28, 2021

MBUNGE WA NGORONGORO WILLIAM OLE NASHA AFARIKI DUNIA

 

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Mbunge wa Ngorongoro, William Ole Nasha amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo jijini Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa Spika Job Ndugai, Wabunge, Familia na Wananchi wa Ngorongoro. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina.

No comments:

Post a Comment

Pages