September 28, 2021

RC Makalla aliagiza Jeshi la Polisi kufanya operesheni ya kuwakamata wezi wa vifaa vya magari na vibaka Dar

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla.

 


Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla ameliagiza Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam kuanza msako wa kuwabaini na kuwakamata Wezi wa Vifaa vya Magari Na vibaka na kuwachukulia hatua Kali za kisheria.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa Kikao Cha tathimini ya ziara yake ya kusikiliza Migogoro Jimbo kwa Jimbo ambapo amesema kumeanza kuibuka vitendo vya wizi na kuleta taharuki kwa wananchi jambo ambalo hawezi kulifumbia macho.

Aidha RC Makalla ametoa wito kwa wazazi kuchunguza mienendo ya watoto wao na kuwakanya ili wasijekuingia kwenye mikono ya vyombo vya dola.

Agizo hilo limetolewa kwa mikono miwili na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam  Jumanne Muliro ambae amewaelekeza makamanda wote wa Mikoa ya kipolisi kuanza kazi ya kuwasaka wahalifu mara moja.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa mkoa huo, Hassan Rugwa amempongeza RC Makalla kwa ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi na kwamba ufanyaji tathmini ya wamachinga unaendelea lengo likiwa kuwatafutia maeneo bora ya kufanyia biashara zao.



No comments:

Post a Comment

Pages