September 03, 2021

JAMII YATAKIWA KUWAUNGA MKONO WANAWAKE KUSHIKA NAFASI ZA UONGOZI


 Mratibu wa mradi huo kutoka ZAFELA Khairat Hamid akifungua mkutano wa waandishi wa habari. Katikati ni Mkurugenzi wa ZAFELA Jamila Mahmoud na mwengine ni mratib wa mradi huo kutoka TAMWA-ZNZ Salma Amir Lusangi.


Na Talib Ussi, Zanzibar

 

Mkurugenzi wa Jumuia ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) Jamila Mahmoud Juma amesema wamepanga kufanya   mkutano maalumu utakaolenga kuihamasisha jamii kuwaunga mkono wanawake kushika nafasi za uongozi.

 

 

Aliyasema hayo mbele ya  waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho zilizopo Mpendae  visiwani humu na kubainisha kuwa mkutano huo utafanyika katika  viwanja vya kisonge Jumapili ya septemba 5 mwaka huu mjini Unguja.

 

Alifahamisha kuwa mara baada ya mkutano huo aliupatia jina la mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya wanawake kushiriki katika uongozi mikutano mengine itafanyika kila wilaya Zanzibar nzima.

 

Jamila alieleza kuwa katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili wanawake katika kutafuta nafasi za uongozi wanadhani mikutano hiyo ni njia madhubuti ya kuwahamasisha na wao kujitoa kwa moyo mmoja.

 

 

Awali mratibu wa mradi huo kutoka TAMWA-ZNZ Salma Amir Lusangi alisema mradi huo unalenga kuwafikia wanawake elfu sita kutika wilaya zote za Unguja na Pemba.

 

Alisema mradi huo  wa miaka mine unatekelezwa na TAMWA-ZNZ kwa  kwa kushirikiana na PEGAO pamoja na ZAFELA chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Norway Nchini Tanzania.

 

 Mkutano huo ambao umelengwa kuwaamsha wanawake kujua haki zao katika kupugani nafasi za uongoz Mgeni Rasmin atakuwa  Waziri wa TAMISEMI Massoud Ali Mohamed, .

No comments:

Post a Comment

Pages