September 03, 2021

TRA: Umakini waongezeka katika kukusanya kodi vyombo vya moto

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetilia mkazo katika ukusanyaji wa mapato katika ubadilishwaji/umiliki wa chombo cha moto.


Afisa Msimamizi wa Kodi Maya Bakari  Magimba amesema, ubadilishwaji umiliki unapashwa kufuata vigezo vilivyowekwa na TRA ili kumpatia uhalali.


Maya anasema nyaraka zinazotakiwa na TRA ili kukakilisha ubadilishaji wa umiliki kuwa ni pamoja na barua ya kuomba umiliki mpya, kitambulisho, pasipoti moja(picha), mkataba wa majununuzi toka kwa manasheria, risiti wa EFDs.


Nyaraka nyingine ni TIN ya mmiliki mpya, chombo kupelekwa TRA kuonwa, kulipia kodi za kuamisha umiliki(chombo husika) na kulipia kodi mpya.


Mapema akifungua semina ya kuhusu mabadiliko ya sheria ya kodi kwa mwaka 2021,  Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi  (TRA) Richard Kayombo amesema uongozi wa mamlaka hiyo umedhamiria kuwatumikia wananchi na kuyatekeleza maagizo yote aliyoyatoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ili kukusanya mapato kwa Serikali.


Kayombo amesema, kati ya maagizo aliyoyatoa Rais Samia ni pamoja na ukusanyaji wa kodi kwa haki pamoja na kupanua zaidi wigo wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali. 


Amesema TRA imekuwa ikifanya ushirikishaji wa aina mbalimbali kwa wananchi kwa lengo la kukusanya mapato kwa kuzingatia  weledi, haki pamoja na kusimamia kazi zake kwa weledi ili kufikia lengo la kukusanya kiwango cha Sh Trill 22.88 ambacho kimeelekezwa na Serikali.


Ameongeza kuwa, uboreshaji huo umehusisha pia mashine za kielektroniki (EFD's) ambazo awali zililamikiwa sana na wafanyabiashara na kusababisha kuwapo kwa risiti za kughushi.


Amesema kutokana na kuwapo kwa wimbi la Ugonjwa wa Virusi vya COVID 19,  TRA imefanikiwa kuanzisha huduma kwa njia ya mtandao kama njia ya kuepuka misongamano katika Ofisi za Mamlaka hiyo na kujikinga na maradhi hayo.


Naye Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa DCPC), Irene Mark amesema klabu hiyo imekuwa ikifanyakazi kwa karibu na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo TRA lengo ni kutoa taarifa sahihi kwa wananchi baada ya waandishi hao kupatiwa mafunzo.

 

"DCPC imekuwa mdau mkuu wa taasisi mbalimbali ikiwamo TRA, lengo ni kuwezesha waandishi kufikisha ujumbe na taarifa sahihi kwa wakati."amesema. 

No comments:

Post a Comment

Pages