HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 01, 2021

NMB MARATHON 2021 YAZIDI KUNOGA

*Wanariadha nyota, Simbu, Failuna wajitosa
*Sh. Bilioni 1 kukusanywa kusaidia akina mama wenye fistula CCBRT


Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini, Dismas Prosper (kulia), akiwaelekeza wanariadha maarufu nchini, Felix Simbu na Failuna Matanga (kushoto) namna ya kujisajili kwa njia ya mtandao kwa ajili ya kushiriki mashindano ya NMB Marathon 2021 jijini Dar es Salaam mwezi huu. (Na Mpiga Picha Wetu).


Meneja wa benki ya NMB Kanda ya Kaskazini, Dismas Prosper (kulia), akimwelekeza Failuna Matanga namna ya kujisajili kwa njia ya mtandao kwa ajili ya kushiriki mashindano ya NMB Marathon 2021 jijini Dar es Salaam mwezi huu, kushoto ni Meneja wa tawi NMB Clock Tower jijini Arusha,Emmanuel Kishosha.

 


Na Mwandishi Wetu, Ausha

WANARIADHA mahiri nchini walioiwakilisha Tanzania kwenye Michezo ya Olimpiki Tokyo, Japan, Alphonce Felix Simbu na Failuna Abdi Matanga wamejitosa rasmi kushiriki mbio zilizoandaliwa na Benki ya NMB zijulikanazo kama NMB Marathon zinazotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam, Septemba 18 , 2021.

Wanariadha hao, wamejisajili rasmi Jijini Arusha  katika tawi la NMB Clock Tower.

Katika michuano ya Olimpiki Tokyo, wanariadha hao walishiriki katika Mbio za Full Marathon Km. 42.195 ambapo kwa wanaume, Simbu kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania akishika nafasi ya Saba huku Failuna anayetokea Talent Club akiibuka wa 24 kwa upande wa wanawake.

Akizungumza Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini, Dismas Prosper,  ameeleza mbio hizo za hisani zina malengo ya kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kuchangia tiba  ya akinamama wenye matatizo ya fistula, Kwa ushirikiano na Hospitali ya CCBRT, ambao wamekuwa na changamoto ya magonjwa hayo na kushindwa kupata fedha kwa ajili ya  matibabu.

Meneja huyo wa Kanda,  amesema Wananchi wengine wakijiunga kujisajili kushiriki mbio hizo, watakuwa wamesaidia ukusanyaji wa kiasi hicho cha  fedha ili kuwapa tumaini Watanzania walio na changamoto ya ugonjwa huo.

Kwa upande wao wanariadha, akiwemo Failuna na Simbu walisema
wanaimani kubwa akinamama wakisaidika itakwenda kupunguza changamoto na idadi kubwa ya Wanawake wanaoishi na Fistula.

"Sisi tunajifua kwa ajili ya kushiriki mbio hizi zenye lengo zuri la kuimarisha afya za washiriki na pia kutibu wenye matatizo ya fistula," alisema Simbu.

Katika kuhakikisha mashindano hayo yanafana Chama cha Riadha Mkoa wa Arusha (ARAA), kupitia Katibu Mkuu wake, Rogart John Steven Akhwari, amesema wanayo furaha kubwa kwa NMB kuandaa mbio hizo zenye mlengo wa kuigusa jamii na wapo bega kwa bega  kushiriki, kwani klabu zote za michezo mkoani humo zimethibitisha ushiriki na idadi kubwa ya Washiriki wameendelea kujitokeza kujisajili ili kwenda jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mbio hizo.

No comments:

Post a Comment

Pages