Na John Marwa
UONGOZI wa Klabu ya Yanga umethibitisha kuachana na aliyekuwa Ofisa Mhamasishaji na Msemaji wa Klabu hiyo Anthonio Nugaz (pichani).
Kwa mujibu wa taarifa ya Klabu hiyo iliyotufikia jioni hii imeeleza kuwa maamuzi hayo yamefikiwa baada ya mkataba wake wa miaka miwili kumalizika.
Taarifa hiyo imetoka shukrani za dhati kwa Nugaz kwa utumishi wake alioitymikia Yanga SC.
"Uongozi wa Klabu ya Yanga unatoa shukrani za dhati kwa aliyekuwa mfanyakazi wake Juma Khatibu Nugaz, maarufu kama Anthonio Nugaz kwa utumishi wake ndani ya klabu ya Yanga katika kipindi cha miaka miwili.
"Ndugu Juma Nugaz amemaliza mkataba wake wa utumishi katika klabu ya Yanga, hivyo Uongozi umeamua kutoongeza mkataba huo na kwamba unamshukuru sana kwa kazi yake na kumtakia kila la heri na mafanikio katika maisha na kazi zake nje ya Klabu ya Yanga." Imeeleza taarifa hiyo.
No comments:
Post a Comment