September 02, 2021

NMB yaikabidhi vifaa Bunge Michezo tayari kwa Tamasha la Kivumbi na Jasho Jumamosi hii

 


Afisa Mkuu wa Biashara na Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kushoto) akimkabidhi jezi Mwenyekiti wa Bunge Sports Club, Mhe. Abass Tarimba (katikati) kwa ajili ya Tamasha la NMB na wabunge litalofanyika jumamosi katika viwanja vya Jamhuri na Chinangali Park jijini Dodoma. Kushoto ni Mwakamu Mwenyekiti, wa Bunge Sports Club Mhe. Esther Matiko.


Afisa Mkuu wa Biashara na Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kushoto) Mwenyekiti wa Bunge Sports Club, Mhe. Abass Tarimba (katikati) na Makamu Mwenyekiti, wa Bunge Sports Club Mhe. Esther Matiko wakionyesha mipira itakayotumika kwenye  ya Tamasha la NMB na Wabunge litakalofanyika jumamosi katika viwanja vya Jamhuri na Chinangali Park jijini Dodoma.


Afisa Mkuu wa Biashara na Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kushoto) Mwenyekiti wa Bunge Sports Club, Mhe. Abass Tarimba (katikati) na Makamu Mwenyekiti, wa Bunge Sports Club Mhe. Esther Matiko wakionyesha jezi zitakazotumika kwenye  ya Tamasha la NMB na Wabunge litakalofanyika jumamosi katika viwanja vya Jamhuri na Chinangali Park jijini Dodoma.
 

Afisa Mkuu wa Rasilimaliwatu NMB, Emmanuel Akonaay, Afisa Mkuu wa Biashara na Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (katikati) pamoja na Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Juma Kimori wakionyesha sehemu ya vifaa vya michezo (jezi na mpira) vitakavyotumika kwenye Tamasha la NMB na Wabunge litakalofanyika jumamosi katika viwanja vya Jamhuri na Chinangali Park jijini Dodoma.


Na Mwandishi Wetu

 

Benki ya NMB, leo imekabidhi vifaa vya michezo kwa timu saba za Bunge Sports Club, zinazoundwa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwaajili ya Tamasha la la NMB na Bunge lenye kauli mbiu ya Kivumbi na Jasho. Vifaa hivyo ni pea 20 za tracksuit, seti moja ya jezi za netiboli, pisi 15 za mpria ka kikapu, mipira 6, pea 16 za jezi za soka, pea 10 za jezi za mchezo wa kikapu (wanawake), jezi za kukimbilia pisi 200 - vyote vikiwa na thamani ya Sh. Mil. 12.

 

Michezo hiyo itafanyika baina ya Waheshimiwa Wabunge na Wafanyakazi wa Benki ya NMB ikiwa pia ni maandalizi ya mbio za NMB Marathon 2021- Mwendo wa Upendo zitakazo fanyika jijini Dar es Salaam tarehe 18 mwezi huu.

 

Tamasha la Kivumbi na Jasho, linatarajia kufanyika Jumamosi Septemba 4, kwenye viwanja vya Jamhuri na Chinangali Park jijini Dodoma.

 

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, alisema licha ya kutumika kujenga mahusiano mema baina ya taaisi hizo, tamasha hilo ni sehemu ya juhudi za Benki ya NMB kuhakikisha jamii ya Kitanzania inapenda michezo, ambayo ni muhimu kwa afya na pia ni ajira.

 

Alisema wanajisikia furaha kupata nafasi adhimu ya kujumuika pamoja na watunga Sheria hao, ambao Wengi wao ni wateja wao, hivyo wanaushukuru uongozi wa Bunge na Kamati ya Utendaji ya Bunge Sports kwa kukubali kutenga muda wa kushiriki Tamasha hilo.

 

Mponzi alieleza mbele ya Mwenyekiti wa Bunge Sports, Tarimba Abbas ambaye ni Mbunge wa Kinondoni kuwa

watalianza Tamasha la Kivumbi na Jasho kwa mbio za taratibu 'jogging' asubuhi kuanzia viwanja vya Bunge hadi Chinangali Park, kisha michezo mingine ikiwamo kuvuta kamba, kikapu, netiboli, wavu, kukimbiza kuku na mpira wa miguu kisha kukabidhi zawadi washindi.

 

Akitoa neno la shukrani, Tarimba aliipongeza NMB kwa dhamira ya dhati ya kuimarisha mahusiano baina ya taasisi hizo kiasi cha kuwaandalia tamasha hilo na kwamba Spika wa Bunge, Job Ndugai, amesisitiza na kuonesha umuhimu na thamani ya Kivumbi na Jasho, na wao kama wabunge wapo tayari kukiamsha jumapili ili na wao wawe sehemu ya Mwendo wa upendo upendo unaolenga kurejesha tabasamu kwa akina mama wenye matatizo ya Fistula kwani wanaamini Fistula inatibika.

 

No comments:

Post a Comment

Pages