September 02, 2021

Waungeni Mkono wanawake katika kupigania nafasi za uongozi

 

Mtaalamu wa maswala ya habari Tanzania Dkt, Abuubakari Rajab akiwasilisha ripoti juu ya uwakilishi wa habari za wanawake katika vyombo mbalimbali vya habari nchini.

 


Baadhi ya waandishi wa habari wa vyambo mbali mbali Tanzania wakifuatilia ripoti ya wanawake na Uongozi kupitia vyombo hivyo.

 

Na Talib Ussi Zanzibar

 

Chama cha Waaandishi wa habari Wanawake TAMWA-Zanzibar kimevitaka vyombo vya habari nchini kuwaunga mkono wanawake katika kupigania nafasi mbali mbali za Uongozi kwa kupaza sauti zao kupitia vyombo hivyo.

 


kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa chama hicho Dkt, Mzuri Issa Ali huko Tunguu Wilaya ya kati Unguja katika ofisi za Chama hicho katika uzinduzi wa ripoti ndogo ambayo kuangali jinsi gani  vyombo vya habri kama vinatoa uzito kwa kiasi gani habari zinazohusu wanawake na uongozi



Alisema  kwa kuwa vyombo vya habari umuhimu mkubwa katika kupaza sauti ya mwanamke ambao wanajitokeza katika kutafuta nafasi za uongozi katika Serikali ya mapinduzi Zanzibar .



Alisema vyombo vya habari kupitia mkakati maalumu wanawake kuwaandaa  wanawake kushika nafasi za uongozi kupitia vipindi vyao vya kila siku kwani wanawake ni watu wanaoitaji motisha.

 

Alisema wanawake wengi hawajitokezi kugombea nafasi za uongozi kwa sababu hawajui wajibu wao na kudai kuwa kama vyombo vya habari vitashuka chini na kuweza kupaza sauti basi wengi watapata mwamko wa kuingia kwenye uongozi hasa wa siasa.

 

“ Vyombo vyetu kaama vitaenda vijijini kuwafanyia watu mahojiano na wakaandika habari zinazoonyesha umuhimu wa mwanamke kuwa kiongozi basi wengi wanaweza kiujitokeza” alisema Dr. Mzuri.

 

Aliwaomba waandishi wa habari kutumia kalamu zao katika kumjenga mwanamke kiuwezo wa kugombea naffasi hizo na kuwa juhudi maalum dhidi ya wanawake.

 

 

Akimkaribisha Mkurugenzi huyo Mratibu wa Mradi wa ushirikishwaji wanawake katika uongozi Salma Jumanne Amir Lusang alisema Mradi huo unatekelezwa kwa kushirikiana Tamwa, ZAFELA na PEGAO ambao umefadhiliwa na Norwe

 

Mratibu aliwakumbusha Waandishi wa habari  kutekeleza wajibu wao  kwa kuangalia usawa kijinsi kwani wanawake na wanaume wanahaki sawa katika uongozi



Dkt,Abuubakar Rajab ambaye ni mtaalamu wa habari nchini wakati akiwasilisha alifahamisha kuwa kupitia utafiti wake bado vyombo vya habari Zanzibar na Tanzania kwa ujumla havijampa umuhimu unaostahiki mwanake kwenye uongozi.



Akiwasilisha ripoti hiyo nguli huyo wa habari aliwaasa wahariri wa vyombo mbali mbali vya habari nchini kuangalia namna ya kutoa haki sawa baina ya wanawake na wanaume kwani wote wanahaki ya kuwa viongozi.



Nao wahariri waliohudhuria katika mkutano huo wa kutoa ripoti hiyo walisema kwa kiasi ripoti imewaonyesha ni jisi gani wamekuwa hawawatendei haki wanawake na kuahhidi kulifanyiakazi changamoto hiyo

No comments:

Post a Comment

Pages