September 08, 2021

NMB yatoa misaada ya Mil. 25/- Kigamboni



Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Nyangasa  akionyeshwa mabenchi ya kukalia katika Hospitali ya Kigamboni na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard yaliyotolewa msaada na Benki hiyo.

  

Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vilivyotolewa na Benki ya NMB kwa Wilaya ya kigamboni, ikiwa ni pamoja na Mabenchi ya kukalia wagonjwa katika Hospitali ya Kigamboni, Madawati 50 kwa shule ya Msingi Ungindoni, Mabati 200 kwa Shule ya Msingi Rahaleo na Mabati 180 kwa Shule ya Sekondari Kigamboni vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 24 . Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Nyangas.

 

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Nyangasa akihutubia wakati wa kupokea msaada wa vifaa mbalimbali vilivyotolewa na Benki ya NMB kwa Wilaya ya kigamboni, ikiwa ni pamoja na Mabenchi ya kukalia wagonjwa katika Hospitali ya Kigamboni, Madawati 50 kwa shule ya Msingi Ungindoni, Mabati 200 kwa Shule ya Msingi Rahaleo na Mabati 180 kwa Shule ya Sekondari Kigamboni vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 24. Kushoto ni Meneja wa  NMB Kanda ya  Dar  es Salaam, Donatus Richard.

 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Nyangasa akionyeshwa madawati na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard  yaliyotolewa na Benki ya NMB kwa Shule ya Msingi Ungindoni.  
 
 
Na Mwandishi Wetu
 

Benki ya NMB, imekabidhi misaada yenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 25 kwa Shule tatu za Msingi, moja ya Sekondari na Hospitali ya wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam, pamoja na a Wilaya hiyo, iliyotolewa kupitia mwamvuli wa Program ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).

 

Msaada huo umekabidhiwa na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, kwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatuma Almasi Nyangasa katika hafla iliofanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni na Shule ya Msingi Ungindoni.

 

Shule za Msingi zilizonufaika ni Ungindoni (madawati 50 yenye thamani ya Sh. Mil. 5), Raha Leo (mabati 200 Sh. Mil. 6.4), Kigamboni Sekondari (mabati 180 Sh. Mil. 5.7) na Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni (mabenchi 20 ya kukalia wagonjwa wakati wakisubiri matibabu, Sh. Mil. 8). 

 

Akizungumza katika hafla hiyo, Donatus aliushukuru uongozi wa shule hizo na hospitali hiyo 0kwa kuitambua NMB Kama mshirika sahihi na wa uhakika wa changamoto za elimu na afya, kiasi cha kupeleka maombi yao kwa benki hiyo.

 

Donatus alibainisha kuwa, mahusiano mema ya benki yake na Serikali na jamii Ni miongoni mwa Siri za mafanikio yao yanayoifanya kuwa benki imara na bora nchini, na kwamba ukubwa wa kiasi wanachotoa kusaidia sekta za elimu, afya na majanga kupitia CSR, kunatokana na ukubwa wa faida yao kwa mwaka wa fedha.

 

"Kila mwaka tunatumia asilimia 1 ya faida yetu kutoa misaada ya kijamii katika nyanja hizo, ambapo kwa mwaka huu tulitenga zaidi ya Sh. Bilioni 2, ambazo ndizo hizi," alisema Donatus mbele ya Mhe. Nyangasa na Meya wa Manispaa ya Kigamboni, Ernest Mafimbo.

  

Kwa upande wake, Mhe. Nyangasa aliishukuru NMB kwa kuwa msaidizi mkuu wa changamoto za elimu na afya Kigamboni, ambayo ni miongoni mwa Wilaya changa, yenye bajeti ndogo, huku ikikabiliwa na changamoto kadhaa kutokana na upya wake kiutawala.

 

Misaada hii ni uthibitisho wa namna NMB inavyojali na kuthamini mahusiano mema baina yao na jamii. Ni wazi kuwa kujitoa huku kunakofanywa na benki hii kurejesha sehemu ya faida yao kwa jamii, kunaipa sapoti kubwa Serikali katika kuboresha mazingira ya Elimu na Afya sio tu kwa Kigamboni, bali kote nchini," alisisitiza Mhe. Nyangasa.


No comments:

Post a Comment

Pages