September 28, 2021

SIMBA BADO WANAJITAFUTA


Na John Marwa


Dakika 90 zimetamatika kwa wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa Biashara United na Simba SC kwa suluhu ndani ya Dimba la Karume mjini Musona.

Ulikuwa mchezo wa kwanza kwa timu zote mbili msimu huu wa 2021/2022.

Haikuwa mchezo uliobebwa na ufundi zaidi ya mipira ya juu kutokana na ubovu wa Uwanja uliopitiliza jambo ambalo liliondoa mvuto wa mchezo.

Simba walipata nafasi ya kuondoka na pointi tatu Lakini mkwaju wa penati wa Fantastic Captain John Bocco kuokolewa na mlinda mlango wa Biashara James Setuba.

Bado Simba haijaonyeaha makali yake, wakishindwa kufunga bao katika michezo mitatu mtawalia.
Biashara wao pointi moja waliyoipata leo ni mafanikio kwao kuizua Simba katika Uwanja huo wa Karume huku walipata clean sheet ya kwanza dhidi ya Mnyama.

Michezo mingine iliyopigwa Leo Mbeya City wamefanikiwa kuanza msimu kwa kishindo baada ya kuwalaza wanajelajela Tanzania Prisons kwa bao Moja kwa mtungi.

Kwa upande wa walima zabibu wa Dodoma Jiji FC wao wameichakaza Ruvu Shooting kwa bao Moja kwa bila.

Ligi hiyo itaendelea kesho kwa michezo miwili ambapo Polisi Tanzania watawaalika KMC FC kutoka  jijini Dar es Salaam.

Wakata miwa wa Kagera Sugar watakuwa na kibarua kizito mbele ya Wananchi Yanga SC kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Kagera.
Mwisho

No comments:

Post a Comment

Pages