September 29, 2021

YANGA SC YAONDOKA NA POINTI 3 KAGERA

 

Kikosi cha Yanga.


Na John Richard Marwa


DAKIKA 90 za Mwamuzi Abdalah Mwinyimkuu kutoka Singida zimehitimisha dakika 720 za Michezo nane ya ufunguzi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara TPL msimu wa 2021/2022.

Zilikuwa dakika 90 za haja kunako Dimba la Kaitaba mjini Bukoba kwa Wananchi Yanga SC kuibuka na ushidi mfinyu mbele ya wenyeji wao Kagera Sugar.

Yanga walijiandikia bao lao kupitia kwa Feisal Salumu 'Fei Toto' dakika 33 baada ya uzembe wa safu ya ulinzi ya Kagera Sugar.

Licha ya ushindi huo Yanga bado imeonyesha bado haiko timamu kipindi cha pili wachezaji ni kama wanakuwa nje ya mchezo ama kuishiwa upepo wa kuendelea kupambana.

Mchezo mwingine uliopigwa Leo, Polisi Tanzania wao wameibugiza KMC FC mabao 2-0.

Kwa ushindi huo Polisi Tanzania wamekaa kileleni mwa msimamo nanpointi zao tatu na mabao mawili, nafasi ya pili ni Namungo FC wenye pointi tatu.

Mzunguko wa kwanza umeshuhudia mabao 10 yakiwekwa nyavuni katika michezo nane ya awali, wastani wa bao 1.02.

Mabao 10 katika michezo nane yenye dakika 720 sawa na bao moja Kila baada ya dakika 72 lilikuwa likifungwa bao.

Ndo kwanza kumekucha TPL 2021/2022 yenye timu 16 Sasa bado michezo 29 kwa timu zote.

No comments:

Post a Comment

Pages