September 23, 2021

Simba na Yanga kama Nyani tu wanachekana lakini hawayaoni madhaifu yao japo wanayakumbatia na kuyasujudia


Na John Marwa
 

Kwa mujibu wa repoti ya Bodi ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara TPLB, juu ya takwimu za Klabu zilizoingiza mashabiki wengi kila mmoja ameibuka nanlake na kila mmoja anabaki na anachokiamini japo hapa kuna kuuumia kwa kutojua na kufurahia kwa kutojua.

Mijadala imekuwa mikubwa, walioibuka kidedea wanajipiga kifua na kunusa makwapa na walio pigwa wamebaki kuhuzunika na kuendelea kuamini takwimu yawezekana haziko sawa.

Sasa kwa mujibu wa maelezo ya Ofisa habari wa TPLB ameeleza kuwa takwimu hizo zimepatikana kwa mujibu wa ripoti walizozipokea kutokana na tiketi zilziouzwa kwa mechi husika.

Hivyo basi kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa ligi misimu miwili nyuma klabu mwenyeji wa mchezo ndio anachukia Ile asilimia 60 ya mapato na mgeni haambulii kitu.

Sasa kwa mujibu wa kanuni hiyo na kwa mujibu wa takwimu za TPLB mambo yako namna hii mahabiki 141,681 wa @yangasc ni wale walioingia katika michezo yao ya nyumbani ambayo ilikua 17 msimu uliopita na sio walioingia Yanga akicheza na Biashara pale Karume Musoma licha ya kuwa mashabiki wengi hapa watakuwa waliingia wa Yanga lakini kwenye takwimu hawa ni wa Biashara.

Tukirudi kwenye watazamaji wa Yanga 141,681 tugawe kwa michezo 17 ya Yanga aliyocheza Nyumbani ni sawa wastani wa mashabiki 8,334 kwa mchezo mmoja.

Simba ambao wameingiza mashabiki 138,518 gawanya kwa michezo 17 ya Nyumbani ni sawa wastani wa Mashabiki 8,148 kwa mchezo mmoja wa nyumbani.

Je swali la kujiuliza kabla ya kwenda mbali no wastaniwa mashabiki 800+ ndio wanaoingia kwenye michezo ya Simba na Yanga wakiwa nyumbani.

Ki uhalisia mashabiki wanaohidhuria viwanjani Simba na Yanga zikiwa na cheza na timu nyingine ni wazi ni chini ya mashabiki 500+ namba nyingine zikijaziwa na mechi mbili aidha wenyewe kwa wenyewe ama wakikutana na Azam FC.

Hapa kuna jambo tumejifujza kwamba Takwimu za TPLB sio za kujisifia kwa Klabu yoyote kwa hadhi ya Soka letu lilipo fika sasa.

Ni wazi hakuna watazamaji viwanjani, kuna kazi kubwa inatakiwa kufanyika kuwarejesha mashabiki viwanjani kwani wao ndio wenye mchezo wao.

Ukiangalia tofauti iliyopo kati ya Simba, Yanga na Klabu nyingine utagundua kuwa bado hata hizo namba walizozipata sio za Mashabiki wao parcel.

Kwa mtazamo zaidi naamini kufanya jambo jema ni wajibu usio hitaji hamaki wala msukumo. Kila mmoja akitikiza wajibu wake bila kujali nani anafanya nini naamini tutakuwa kwenye mstari mmoja japo sio lazima kwa sababu ya utu na ubinadamu wetu.

Tulitoe Soka kwenye hamasa twende kwenye matendo katika kila nyanja.

Kongole kwa TPLB kwa kuleta takwimu hizi kuna walio pata furaha ya muda kuna wanao teseka kimyakimya kwa muda lakini jambo jema ni kila mhusika kuchukua hatua kuja kivingine msimu ujao wa TPL 2021/2022.
@johnmarwatz #masterplan✨🌍

No comments:

Post a Comment

Pages