October 11, 2021

Coastal Union yaiendea Mombasa Ruvu Shooting

NA MWANDISHI WETU


TIMU ya Coastal Union ya Tanga kesho Jumaane itacheza mechi ya kirafiki mjini Mombasa nchini Kenya kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Ruvu Shooting.


Coastal Union itajipima nguvu na Bandari FC katika Uwanja wa Tononoka mjini Mombasa.
 

Akizungumzia mchezo huo wa kirafiki Afisa Habari wa Coastal Union, Jonathan Tito amesema  ni sehemu ya kujiweka sawa kabla ya kurejea kwa mechi za Ligi Kuu ya NBC.


"Kipindi hiki cha cha kupisha mechi za timu za taifa vijana wetu walipewa mapumziko ya siku tano, hivyo baada ya kurejea mazoezini tumeona tujiweke sawa dhidi ya majirani zetu Bandari FC kabla ya kuwavaa Ruvu Shooting," alisema Tito.


Coastal Union itaendelea na mzunguko wa tatu wa Ligi Kuu ya NBC  dhidi ya Ruvu Shooting mchezo utakaopigwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi.


Tito amesema mchezo huo dhidi ya Ruvu ni muhimu sana kwa kwao kwa kuwa katika michezo yao miwili ya mwanzo wametoka sare yote wakiwa nyumbani.


"Michezo yetu miwili ya mwanzo dhidi ya Azam FC na KMC FC tumetoka sare, hivyo huu ni mchezo muhimu, hivyo tutapambana tupate matokeo mazuri."

No comments:

Post a Comment

Pages