Na Jasmine Shamwepu, Dodoma
KATIKA Kuadhimisha kilele cha maadhimisho ya wiki ya Posta Duniani Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango ametoa wito kwa uongozi wa Shirika hilo kutumia maadhimisho hayo kurejesha matumaini kwa wananchi kuhusu huduma za posta.
Dk. Mpango ametoa wito huo hii leo jijini Dodoma wakati akifunga rasmi maadhimisho hayo ambapo amewataka watendaji wa posta kuongeza jitihada katika kutangaza huduma zake kote duniani na kutumia zaidi lugha ya kiswahili.
Kwa upande wake Waziri wa Habari Mawasiliano na Keknolojia ya Habari Dkt Ashatu Kijaji ameshukuru na kupongeza jitihada zinazofanyika na shirika hilo pamoja na kusema kuwa anaamini wananchi kote nchini wamefahamu zaidi kuhusu huduma zinazotolewa na shirika hilo kupitia maadhimisho hayo huku Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na uchukuzi Zanzibar Rahma Kassim Ally akiahidi kuboresha huduma za Shirika Hilo kuleta tija kwa Taifa.
Awali Kaimu Posta Masta Mkuu Shirika la Posta Tanzania Macriss Mbodo,amesema lengo la Maadhimisho hayo ni kutambua na kuboresha zaidi huduma za posta kote duniani na kuongeza kuwa shirika hilo limejipanga vyema katika kuboresha huduma ikiwa ni pamoja na kuongeza miundombinu rafiki ya kazi.
Kilele cha maadhimisho hayo kitaifa yamefanyika jijini Dodoma huku mgeni rasm akiwakabidhi vyeti washiriki wa uandishi wa barua pamoja na vitendea kazi kwa kama,magari na pikipiki kwa uongozi wa shirika.
No comments:
Post a Comment