October 11, 2021

Dawa ya kutatua migogoro ya wafugaji na wakulima yaja


 

Meneja wa Kikundi cha K & S Vision cha sanaa  kilipochopo Wilaya Temeke jijini Dar es Salaam Rashid Pazi  akizungumza na waandishi wa habari.

 

  NA ASHA MWAKYONDE, DAR ES SALAAM


MENEJA wa Kikundi cha K & S Vision kilipo Wilaya Temeke jijini Dar es Salaam Rashid Pazi amesema

maandalizi  ya Igizo ambalo linaenda  kutatua changamoto ya migogoro ya wafugaji na wakulima yameshakamilika  kwa asilimia 95.


Igizo hilo ambalo linatarajiwa kumaliza changamoto ya migogoro wafugaji na wakulima linaanzia mkoani Morogoro vijijini na baadae mikoa mingine yenye changamoto hiyo.


Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Pazi amesema maandalizi sio mabaya kwani tarehe waliopanga kwenda mkoani Morogoro haijabadilika.


Pazi ameeleza kuwa hakuna kitu kizuri kama watu kuishi kwa amani hivyo lengo la kuandaa igizo hilo ni kutoa elimu ambayo italeta manufaa kwa jamii hizo za wakulima na wafugaji.


" Watu wa Morogoro watarajie mambo mazuri kwa sababu tunaenda kufanya vitu ambavyo vinaigusa jamii kwani itakuwa ni suluhisho kwa wafugaji na wakulima," amesema Pazi.


Ameongeza kuwa baada ya igizo hilo kuoneshwa wanatarajia kwamba jamii hizo zinataachana na migogoro ambayo inawakosesha furaha na amani na badala yake watakuwa huru kufanya  vitu ambavyo haviwezi kuvunja sheria na kanuni za nchi.

No comments:

Post a Comment

Pages