October 11, 2021

Shirika la Room to Read lawaasa wazazi kuwalinda watoto wa kike

 


Meneja uendeshaji wa miradi kutoka Shirika la Room to Read Tanzania Agripina Kadama akitoa mada wakati wa maadhimisho hayo.



NA VICTOR MASANGU


Wazazi na walezi wametakiwa kuhakikisha kwamba wanawalinda na kuwatunza watoto wa kike ikiwemo kuwapatia haki zao zote za msingi pasipo kuwabagua na kuwapatia stadi za maisha kwa lengo la kuwawezesha kutimiza ndoto zao.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja uendeshaji wa miradi kutoka Shirika la Room To Read Tanzania Agripina Kadama wakati maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani ambayo yamefanyiika jijini Dar es Salaam kwa kuwashirikisha wadau mbali mbali.

Alisema kuwa kwa Sasa watoto wa kike wanatakiwa kuwezeshwa katika Mambo mbali mbali ikiwemo kupatiwa Hali zake za msingi ikiwa sambamba na kupatiwa elimu ambayo itawasaidia katika kutimiza malengo yao.

"Tunaadhimisha siku ya mtoto wa kike duniani lakini kitu kikubwa wazazi na walezi wanatakiwa kutimiza wajibu wao ipasavyo ikiwemo kuwafuatilia mwenendo wao pamoja na kuwapa stadi za maisha ili waweze kujitambua"alisema.

Pia aliongeza kuwa shirika lao kwa Sasa limeweka mifumo mizuri ambayo itawasaidia kupata elimu hasa kwa wanafunzi wa kuanzia miaka 13 Hadi 17 na kwamba wataendelea kuwasaidia wanafunzi kutoka maeneo mbali mbali.

Kadhalika alisema kuwa mtoto wa kike anakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo baadhi yao wanajikuta wanakatisha masomo yao kutoka na wazazi au walezi kuwaozesha wakiwa wadogo.

"Tutaendelea kushirikiana bega kwa bega na serikali katika kuwasaidia watoto wetu wa kike kwa kuwapatia maadili mazuri ya kuweza kujitambua zaidi katika suala zima la kimaisha.

Katika hatua nyingine alisema kuwa mpaka Sasa mradi huo wameshapita katika halmashauri mbali mbali hapa nchini na kubainisha kuwa mradi huo unagusa  masuala ya usomaji na maktaba.

Kwa upande  mkuu wa kitengo Cha elimu kutoka Tamisemi Theresia Kuiwite amesema kwamba serikali itahakikisha kwamba inasimamia Sera zote na mipango inayuhusiana na elimu.

"Sisi Kama serikali tutahakikisha kwamba tunaboresha elimu kwa watoto wa kike pamoja na kutekeleza mipango yote ambayo imewekwa na serikali ikiwemo suala la kusimamoa Sera ya elimu na stadi za maisha kwa wanafunzi.

Kwa upande wake mmoja wa wanafunzi kutoka shule ya Sekondari Bundikani Sifa Mapinduzi amelipongeza shirika la Room to Read Tanzania kwa kumwezesha kupata mafunzo ya stadi za maisha ambayo yameweza kumsaidia kujitambua na kukabiliana na changamoto mbali mbali.

Maadhisho ya siku ya mtoto wa kike duniani kwa mwaka huu kauli mbiu yake  inasema kwamba stadi za maisha ni ufunguo wa ndoto za mtoto wa kike.


No comments:

Post a Comment

Pages