Na Lydia Lugakila, Bukoba
Hoja ya kuumega Mkoa wa Kagera iliyokuwa imepangwa kujadiliwa katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa Kagera, imesogezwa mbele kutokana na unyeti wa hoja hiyo.
Akiahirisha hoja hiyo katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge amesema kuwa kutokana na muda kuwa mfinyu, na kulingana na uzito wa hoja husika ambayo inalenga kutazama upya Mambo ya Msingi yahusuyo Usalama wa Mkoa, Rasilimali, Fursa.
"Kwakuwa muda wa kujadili suala hili, unahitaji muda, Mimi na wenzangu tutapanga kikao maalum kitakachokuwa na majadiliano ya muda mrefu, kwa nia njema kabisa haiwezekani suala hili linahusisha Uchumi na Ulinzi hivyo linahitaji muda, na sio muda mrefu tutawaambia" Amesema Meja Jenerali Charles Mbuge.
Kikao hicho cha Kamati ya Ushauri ambacho kimefanyika katika Ukumbi wa mikutano wa mkuu wa mkoa Kagera, hukaliwa kila baada ya Miezi mitatu ikiwa ni kujadili mipango na maazimio.
October 30, 2021
Home
Unlabelled
Hoja ya kuumega mkoa wa Kagera yaahirishwa
Hoja ya kuumega mkoa wa Kagera yaahirishwa
Share This
![Author Image](http://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgNGvOjyY3CdwpCJ9TBP954xiCYfN1bBZzYpUcDlTp9LIiUwsBaOOVEU6FK0twCpjMrY4dKsssV2e7rNwXCd-dbQVTRyv2njavUJV6cC0A2EcxDUJxTWzqjlrZgaWYsdA/s113/dande.jpg)
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment