Katibu Mkuu wa PRST, Ndege Makura, akizungumza na waandshi wa habari.
Mwanachama wa PRST ambaye pia ni Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara, akizungumza katika mkutano huo.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Chama
cha Maafisa Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST) kimewakumbusha na kuwataka
maafisa uhusiano nchini kufanya kazi kwa kutekeleza majukumu yao kwa
niaba ya taasisi zilizowaajiri na sio watu wanaongoza taasisi hizo.
Aidha,
chama hicho kimewaomba wanahabari kuwasilisha changamoto wanazokutana
nazo kutoka kwa maafisa uhusiano kwa ajili ya kufanyiwa utatuzi kwani
PRST lengo likiwa kuendeleza uhusiano uliopo.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa PRST, Ndege Makura
katika Mkutano Mkuu wa Chama hicho uliofanyika jijini humo.
Amesema
kuwa kumekuwapo na baadhi ya maafisa hao wanaosahau majukumu
wanaotakiwa kuyafanya ndani ya taasisi wanazofanyia kazi kwani hufanya
kazi ya kuwatangaza watu badala ya kufanya kazi kwa niaba ya taasisi
zao.
" Mbrand taasisi sio watu tuhakikishe
tunajikita kufanya kazi kwa niaba ya taasisi si vinginevyo maafisa
uhusiano wanatakiwa kutambua majukumu yao ndani ya taasisi," amesema
Makura.
Amebainisha kuwa wanahabari na
wanachama kuendeleza uhusiano mzuri na kwamba endapo kutatokea
changamoto wasisite kuziwasilisha mbele ya chama hicho kwa utatuzi.
Amesisitiza
kuwa wanahabari na PRST ni vyombo vinavyotegemeana hivyo hakuna haja ya
kukosana na kwamba changamoto zinapotokea wazipeleke kwenye chama
hicho.
Ameongeza kuwa chama hicho kina
wanachama 364 waliopo kazini huku wengine wakiwa katika Vyuo Vikuu
nchini kikiwemo cha Mtakatifu Augustine, Mwanza, Chuo cha Usafirishaji
Tanzania (NIT) na Chuo Kikuu cha Tumaini- Tawi la Dar es Salaam
(TUDARCO).
Amefafanua kuwa katika mkutano huo
umekikutanisha chama hicho na wadau kutoka Serikalin na sekta binafsi na
kwamba wamejadili mambo mbalimbali yaliyojikita kukuza taaluma hiyo.
Kwa
upande wake, Mwanachama wa PRST ambaye pia ni Msemaji wa Klabu ya
Yanga, Haji Manara amesema kupitia mkutano amejifunza mambo mengi
ikiwemo wajibu wake katika taaluma ya afisa uhusiano.
No comments:
Post a Comment