October 08, 2021

TANESCO TABORA WAHIMIZWA KUFANYA KAZI KWA BIDII


Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Tabora Mhandisi Saidi Msemo akimlisha keki mmoja wa wateja kwenye maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja. 
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Tabora Mhandisi Saidi Msemo akimlisha keki mmoja wa wafanyakazi wa shirika hilo teja kwenye maadhimisho hayo. 
Sherehe zikiendelea.
Sherehe zikiendelea.
Shamra shamra zikiendelea.
 


Na Mwandishi Wetu, Tabora

 

 MENEJA wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Tabora Mhandisi Saidi Msemo amewataka wafanyakazi wa shirika hilo kuongeza kasi ya kufanya kazi zaidi.

Msemo ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wafanyakazi hao katika maadhimisho ya siku ya  Huduma kwa Wateja.

"Nitumie siku hii ya maadhimisho kuwaomba muongeze bidii ya kufanya kazi sina maana hamfanyi kazi bali ongezeni bidii zaidi,". alisema Mhandisi Msemo.

Msemo alisema hivi sasa Shirika hilo limeboresha huduma zake ikiwa ni pamoja na kuondoa ukatikaji wa  umeme.

Msemo alitaka huduma za kuwafungia umeme wateja wao  zifanyike ndani ya kipindi cha wiki mbili.

Alisema mteja akisha kamilisha taratibu zote za kuingiziwa umeme apatiwe namba ya kumbukumbu ya malipo (Control No) kwa wakati na kuwa  jambo hilo atalifuatilia kwa karibu kwani hivi sasa shirika hilo ni jipya.

Baadhi ya wafanyakazi waliohudhuria sherehe hiyo ambayo ilikwenda sanjari na kukata keki walisema maadhimisho hayo yamewaongezea ari ya kufanya kazi kwa bidii na lengo likiwa ni kuwatumikia wananchi.

Maadhimisho hayo yalikwenda sambamba na utoaji huduma kwa wateja waliokuwepo ofisini hapo kwa mahitaji tofauti ambapo walipatiwa mafundi wa vitengo husika na kwenda kufanyiwa kazi.

Katika maadhimisho hayo wateja waliweza kuuliza maswali na kueleza mahitaji yao kama ya kucheleweshewa kupimiwa na kupatiwa namba ya kumbukumbu ya malipo ambayo yalitafutiwa ufumbuzi papo hapo.

Mmoja wa wateja aliyejitambulisha kwa jina la Mirambo alilipongeza shirika hilo kwa kuwajali wateja wao kwa kuwapa huduma kwa wakati.

No comments:

Post a Comment

Pages