October 07, 2021

TFF yaingia Mkataba wa Miaka mitatu na NBC kudhamini Ligi Kuu Tanzania Bara, kuitwa NBC Premier League


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi rais wa TFF Wallace Karia wakionesha mkataba wa Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu wenye thamani ya shilingi bilioni 2.5 uliosainiwa leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi na Rais wa TFF Wallace Karia wakisaini Mkataba wa Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu Bara wenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.5.
 
 
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limeitambulisha Benki ya Taifa ya Biashara Nchini (NBC) kuwa Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu Tanzania Bara Msimu wa 2021/22 kwa kutiliana saini mkataba wenye thamani ya Sh Bilioni 2.5.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba huo Rais wa TFF, Wallace Karia amesema kwa sasa ligi hiyo itafahamika kwa jina la NBC Premier League kwa kuwa benki hiyo ni wadhamini wakuu hivyo mchanganuo wa fedha utatumika kwenye usafiri.

Amebainisha kuwa ligi kuu imeanza kutimua vumbi pasipokuwa na mdhamini na kwamba kwa kipindi cha miaka mitatu ligi hiyo itaitwa jina hilo huku akisisitiza kuwa ni mwendelezo wa kuiboresha.

" Wakati wadhamini wa kwanza wanaingia ligi kuu madhumuni makubwa  ilikuwa kusaidia usafiri wa kwenda na kurudi kwenye vituo vya mechi vya timu shiriki hakukuwa na tatizo la timu kushindwa gharama za usafiri," amesema Karia.

Ameongeza kuwa wa hawajabadili kitu kwani sehemu kubwa ya fedha hiyo itasaidia vilabu kwenye suala la usafiri na kwamba sehemu ya mishahara imeshashuhulikiwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi amesema wamefarijika kuingia udhamini kwa kuwa mchezo wa mpira unafuatiliwa sana hapa nchini na kwamba kwa mujibu wa CAF ligi kuu ipo nafasi ya 8.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Theobald Sabi na Rais wa TFF Wallace Karia wakisaini Mkataba wa Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu Bara wenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.5(1).

No comments:

Post a Comment

Pages