October 07, 2021

UPR yawakutanisha THDRC, THBU na Serikali kujadili mapekekezo 133 ya Haki za Binadamu kuelekea Mkutano wa Uswizi


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpangu akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika Kikao cha UPR kilichowakutanisha THDRC, THBU na Serikali kilichojadili mapendekezo mbalimbali ya Haki za Binadamu.

 

 

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini (THRDC) umekutana na wadau mbalimbali wa kutetea haki za binadamu na taasisi za Kiserikali  ikiwa ni siku chache kabla ya kufanyika kwa mkutano wa ujadiliwaji na upitishwaji haki hizo na utekelezwaji wake utakaofanyika nchini  Uswizi Novemba 5 mwaka huu.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu Mzunguko wa Tatu wa Mchakato wa Kimataifa wa Mapitio ya Hali ya Haki za Binadamu (UPR] Naibu Katibu Mkuu wa  Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju amesema kuwa kikao hicho ni maandalizi ya kuelekea Mkutano wa Uswizi pia kitajadili mapendekezo 133 kuhusu haki za binadamu  ambayo serikali imeyaridhia na utekelezaji wake katika kipindi cha miaka minne ambapo pia katika kikao hicho Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora(THBU) ambayo ni taasisi ya serikali imeshiriki.


 Amebainisha kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali katika kupigania haki za binadamu hapa nchini ambapo mapendekezo ambayo kama nchi imeyaridhia kuhusu haki za binadamu pia itajadiliwa taarifa inayohusu utekelezwaji huo na serikali itatuma wawakilishi katika mkutano unaotarajiwa kufanyika nchini humo.


Kwa upande wake, Mratibu wa kitaifa wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania THRDC Wakili Onesmo Olengurumwa amesema kuwa mwaka 2016 Tanzania ilipata karibia mapendekezo 290 Tanzania na  ikakubali mapendekezo 133,na kuongeza kuwa mkutano huo utajadili kama nchi katika mapendekezo iliyoyakubali imetekeleza mangapi na kwa kiasi gani na baadaye watatoa mapendekezo mengine na kwamba kinachofanyika t ni kuangalia Mkutano huu katika hayo 133 Tanzania imeweza kutekeleza mangapi, pia hapo hapo tunatoa mapendekezo mengine kwa ajili ya mapitio mengine ambayo yanatarajiwa kufanyika Novemba 4, 2021


Amesisitiza kuwa wao kama watetezi wa haki za binadamu wataendelea kushirikiana na Serikali katika masuala yanayohusu haki za binadamu na utekelezwaji wake.


Nae, Kaimu Katibu Mtendaji wa tume hiyo,Nabor Assey amesema kuwa tume hiyo imekuwa ikishirikiana na wadau wa haki za binadamu hapa nchini kwa kuhakikisha kunakuwepo na haki katika maeneo mbalimbali sambamba na kuwa na mashirikiano na mtandao huo na mashirika mengine tangu mwaka 2018 na wamekuwa

wakishirikiana katika mambo mbalimbali ikiwemo Uanzishaji na uwezeshaji utekelezaji wa shughuli zinazolenga kulinda na kukuza haki za makundi maalumu ya wanawake, watoto na watu wenye ulemavu na ubadilishanaji uzoefu na utaalamu katika michakato mbalimbali ikiwemo utayarishaji na uthibitishaji wa taarifa, uwasilishaji na usambazaji wa mapendekezo ya Universal Periodic Review (UPR) kwa umma.


Kikao hicho cha siku moja kilichowakutanisha wadau kutoka mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu na yale ya umma kimeratibiwa na mtandao wa watetezi wa haki za binadamu  THRDC kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC na shirika la Save The Children Tanzania .


Universal Periodic Review (UPR) ni mchakato wa kila baada ya miaka minne ambao upo chini ya Umoja wa Mataifa, ofisi ya Haki za Binadamu ambapo kila baada ya miaka minne Taifa linapitiwa kuhusu utekelezaji wa haki za binadamu au mapendekezo ambayo yalitokana na mapitio yaliyopita na jinsi gani kama nchi imeyatekeleza na kwa kiwango gani

No comments:

Post a Comment

Pages