October 01, 2021

ZOEZI LA KUWAFUATA WANANCHI KATIKA MIKUSANYIKO KUWAELIMISHA NA KUWACHANJA KWA HIARI KUANZA RASMI WILAYANI KYERWA



Afisa Afya Wilaya ya Kyerwa Yasin Mwinory.


Na Lydia Lugakila, Kyerwa


Hayo yamebainishwa na afisa afya wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera Yasin Said Mwinory katika kikao maalum cha baraza la madiwani kilichofayika katika ukumbi wa  halmashauri hiyo.


Mwinory amesema wilaya hiyo imefanikiwa katika kutoa elimu iliyoendana na uchanjaji huku wakielekeza mafanikio hayo katika kuanza kuwafuata wananchi katika maeneo yenye mikusanyiko ikiwemo kwenye magulio kuwapatia elimu kuwachanja papo hapo watakaokuwa wameridhia kuwa wilaya ya Kyerwa.


Amesema wilaya ya Kyerwa  ilipokea mgawo wa dozi 5,000 ya  UVICO -19 ambapo hadi sasa wananchi walioitikia zoezi hilo ni 1967 sawa na asilimia 48.2 ya walengwa waliokusudiwa kuanzia umri wa miaka 18 na kuendelea.


" Kati ya wananchi ambao wamechanja wanawake ni 843 ambapo muitikio wa wanaume ni mkubwa zaidi ambapo tangu zoezi hili kuanza elimu ya kutosha juu ya chanjo hiyo imetolewa ndo maana mafanikio yanaonekana ambapo Kati ya Septemba 26- 27 mwaka huu wamechanja wananchi 563 ndani ya siku 2" alisema afisa huyo.


Aidha amewaomba wananchi hao kutoa ushirikiano ili kufanikisha zoezi hilo la ki hiari kwa ajili ya afya zao.


"Nimeitikia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suruhu Hassan na baada ya kutupatia chanjo nimechanja tayari sijapata madhara yoyote chanjo ni salama wapuuze wanaotoa taarifa za upotoshaji" alisema Mwinory.


Hata hivyo kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kyerwa Rashid Mwaimu amewashukuru wananchi wilayani humo kwa muitikio wa kupata chanjo hiyo na kuahidi kuendeleza mkakati wa kuhakikisha kuanzia ngazi ya  kitongoji, Kijiji kata hadi tarafa wapelekewa huduma hiyo lengo likiwa ni kupunguza mwendo mrefu kwa wananchi wakati wa kufuata huduma hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages