October 01, 2021

GEITA WAING'ATIA MENO YANGA SC

KLBAU ya Geita Gold FC baada ya kupoteza mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara TPL 2021/2022 dhidi ya Namungo FC Sasa macho na masikio yao ni kuwakabili Wananchi Yanga SC jumamosi hii.


Geita walipoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Namungo mtanange wa ufunguzi wa msimu huu.


Akizungumza kuelekea mchezo dhidi ya Yanga hapo jumamosi Katibu Mkuu wa klabu hiyo Levinus Mtale amesema timu inaendelea na mazoezi baada ya kutoka mkoani Lindi.


"Tunaendelea vizuri, vijana wako vizuri na tunaendelea na mazoezi kuelekea mchezo dhidi ya Yanga na tunaamini tutaibuka na ushindi.


"Kuhusu jezi zetu zilichelewa kidogo hasa za Mashabiki ila tunaamini wiki ijayo zitakuwa zimefika, hivyo tunawakaribisha wafanyabaishara waweze kuwa tayari kuuza jezi zetu.


Geita Gold FC ikumbukwe wamepanda Ligi Kuu msimu huu na michezo yao miwili wameanzia ugenini dhdi ya Namungo na Yanga ambao watakwatuana hapo jumamosi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.


"Baada ya mechi yetu dhidi ya Yanga tutarudi nyumbani kwa mchezo wa kwanza wa msimu tukiwa nyumbani ambapo mechi zetu za nyumbani tutatumia Uwanja wa Ntankumbu Girls, ulikuwa na malekebisho kidogo ila sasa yamekamilika.


"Nafikiri Uwanja Wetu tunaoujenga utakamilka kabla ya Ligi kuisha, Sasa ujenzi wa Majukwaa na upandaji wa nyasi ndio zoezi linaloendelea."amesema na kuongeza kuwa 


Kama Uongozi tunaamini tuna kikosi amabcho kitaenda kutupatia furaha licha ya kuanza vibaya. Lakini niwahakikishie wakazi wa Kanda ya Ziwa timu yao iko tayari kuwapa furaha." Amesema. 

No comments:

Post a Comment

Pages