Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka Akizungumza na wananchi wa kata ya Tumbi.
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Koka ametoa fedha
hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuweza kusikiliza
kero na changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi wa kata ya tumbi
ikiwa sambamba na kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo
Akizungumza
katika mkutano na wananchi wa kata ya tumbi Koka alisema kwamba lengo
lake kubwa ni kuwasaidia vijana waweze kuondokana na wimbi la umasikini
na kuwaletea tija katika kuleta Chachu ya kimaendeleo.
"Mm
Kama Mbunge wenu lengo langu ni kuwasaidia wananchi na wakati nipo
katika kampeni zangu kwa ajili ya kuomba kura niliweza kukiahidi kikundi
hiki Cha boda boda Cha Mwanalugali kukipa mtaji wa fedha ambao
itawasaidia katika kazi zao,"alisema Koka.
Pia
Koka alisema kwamba mbali na kunisaidia kikundi hicho aliongeza kuwa
atahakikisha anaweka mikakati madhubuti ya kuwasaidia wananchi katika
sekta mbali mbali ikiwemo elimu pamoja na afya.
Pia
Mbunge huyo katika kuchochea Kasi ya maendeleo aliweza kuchangia kiasi
Cha shilingi laki tano kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa ofisi ya
serikali ya mtaa wa boko temboni.
Katika
hatua nyingine aliongeza kuwa atashirikiana na mamlaka mbali mbali ili
kuweza kuwasogezea huduma za maji,umeme,pamoja na suala zima la
upatikanaji wa madawa na vifaa tiba katika zahanati ili kuwapunguzia
adha wananchi ya kufuata huduma mbali.
Kadhalika
aliwahakikishia wananchi wa mitaa mbali mbali iliyopo kata ya tumbi
kuwaboreshea zaidi miundombinu ya barabara ili ziweze kupitika kwa
urahisi hasa wakati wa kipindi Cha mvua.
Nao
baadhi ya wananchi waliohudhulia katika mkutano huo wamemuomba Mbunge
kuwasaidia kwa Hali na Mali upatikanaji wa huduma ya nishati ya umeme
pamoja na ujenzi wa kituo cha Polisi na soko.
Kwa
upande wake Diwani wa kata ya tumbi Raymond Chokala alimpongeza Mbunge
huyo kwa kufanya ziara ya kutembelea miradi mbali mbali pamoja na
kutekeleza ilani ya Chama kwa vitendo ikiwemo kuchangia Kasi ya
maendeleo.
No comments:
Post a Comment