Afisa Mwandamizi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Doto Balele (kushoto), akikabidhiwa fomu ya kuomba kugombea nafasi ya Spika na Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Oganizetion CCM Taifa, Solomon Itunda kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Halmashauri kuu ya Taifa (NEC),CCM Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka.
Na Asha Mwakyonde, Dodoma
AFISA Mwandamizi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Doto Balele amechukua fomu ya kuomba kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa amevutiwa na uongozi wa Rais Samia Suluhu Hasaan kwa namna anavyoingoza nchi.
Akizungumza mara baada ya kukubidhiwa fomu hiyo leo jijini Dodoma Januari 13, 2022, na
Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Oganizetion CCM Taifa, Solomon Itunda kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Halmashauri kuu ya Taifa (NEC),CCM Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka endapo atapata nafasi ya kuwa Spika atakwenda kutatua changamoto mbalimbali kwa wananchi.
Amesema uamuzi huo wa kuchukua fomu ni baada ya kuona wanawake wanaweza kushika nafasi za juu na kufanya vizuri ambapo anatolea mfano kwa Rais Samia ambaye anaongeza nchi.
Doto ameongeza kuwa Rais Samia amewapa mwamuko na kuwa tia nguvu wanawake kwa utendaji wake.
Afisa huyo Mwandamizi ameeleza kuwa uwezo wa kuongoza Bunge anao na pia sifa za kugombea anazo kwa kuwa ni haki yake kugombea nafasi hiyo ya juu kwa mujibu wa katiba.
" Bunge linaongozwa kwa mujibu wa katiba na kanuni hivyo nitaenda kuzisimamia na kutakuwa na demokrasia bungeni endapo nitapata nafasi hii nitahakikisha natendea haki," amesema.
Pia amemshukuru Rais Samia kwa kazi nzuri anayofanya yenye maslahi ya Watanzania na kumuombea Mungu ampe afya njema.

No comments:
Post a Comment