HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 22, 2022

Bashe: hakuna mtanzania atakaye kufa njaa


Waziri wa Kilimo Hussein Bashe katika kikao na wasambazaji  wa mbolea kwa lengo la kujadili bei ambayo inampa unafuu mkulima.

 

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

WAZIRI wa Kilimo Hussein Bashe amesema hakuna Mtanzania atakayekufa njaa serikali  ina akiba ya chakula cha kutosha tani 200,000, za mahindi.

Hayo aliyasema jana jijini Dodoma alipokutana na wasambazaji wa mbolea kwa lengo la kujadili bei ambayo inampa unafuu mkulima,Bashe alisema hawatawapa wafanyabiasha wauze tani hizo za mahindi.

Alisema serikali kupitia Halmashauri husika watafungua vituo na mahindi yatauzwa kwa bei ambayo ni nafuu ili wananchi waweze kukidhi na kupata mahitaji yao.

" Wananchi ambao wanaakiba ya chakula waendelee kuhifadhi  kwa sababu tunaweza tusipate chakula kama mwaka jana, tathimini ya awali inaonesha uzalishaji wetu pamoja na upungufu wa mvua  tulikuwa na wastani wa asilimia 125 hadi 127 lakini kipindi hiki kinaweza kushuka kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa," alisema Bashe.

Waziri Bashe aliongeza kuwa kama serikali wanafahamu  bei ya mbolea imepanda na msimu wa mvua za vuli zimeanza kuna baadhi ya wakulima walitarajia kupanda lakini kuna upungufu wa mvua.

" Baadhi ya maeneo nchini mvua zimeanza  kunyesha za masika Taarifa za Mamlaka  ya hali ya Hewa Tanzania (TMA), zinatarajiwa mwezi huu mwishoni kutakuwa na mvua hadi Februari," alieleza.

Alisema maeneo ambayo ni ya mvua chini ya wastani serikali imeanza kuchukua hatua ya kuhakikisha njia mbadala za zao ambalo linaweza kuwasaidia wakulima kupata kipato.

Bashe alifafanua kuwa tayari Serikali imegawa mbegu za alizeti katika maeneo yenye mvua za wastani  zaidi ya tani 1600.

"Tutaendelea kusisitiza na kuwataka wakuu wa mikoa ya maeneo ambayo hayana mvua za kutosha kuhakikisha taarifa wanazozipokea  za hali ya hewa kwa maaneo amabayo hayana mvua,"alisema Bashe.

Aliongeza kuwa maeneo mingine ambayo yana mvua chini ya wastani waendelee kuwasiliana na wizara kwa ajali ya kuendelea kuwapatia mbegu ambazo watazigawa kwa wakulima waweze kupata zao ambalo litawapatia kipato na yenye kustamili ukame.

Waziri huyo alisema wametoa miongozo aina ya mazao ambayo yanaweza kuvumilia ukama yakiwamo mtama na mihogo.
katika kila mikoa.

Aliongeza kuwa serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imetoa ruzuku ya thamani ya bilioni 61 msimu uliopita.

Bashe alisema uzalishaji wa chakula umekabiliwa na bei ya mbolea na serikali inafahamu miaka ya 2015 hadi 2017 ilikuwa ikitoa ruzuku za pembejeo .

" Leo (Jana),tumekutana na wasambaji kuangalia bei inavyokwenda.Tumeanza majadiliano na kampuni za usambazaji wa pembejeo, " alisema Bashe.

Alieleza kuw bei ya mbolea inatokana na mabadiliko ya dunia na kwamba majadiliano hayo yanaweza kufanya bie kushuka.

Waziri huyo aliongeza kuwa wanakabiliwa na changamoto ya hali ya hewa na mbolea kwa maelekezo ya Rais suala hilo linafanyiwa kazi  mapema na kuwapatia wakuli  majawabu ya uhakika.

"Tunawaza kuwa hofu ya kupungukiwa na uzalishaji lakini sio njaa ya kwa binadamu kwa kuwa tumeshajiandaa tuna chakula Cha kutosha," alisema Bashe.

No comments:

Post a Comment

Pages