Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Mahakama
ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ) imetoa mafuzo kwa maafisa wa
mahakama hiyo wa Tanzania wakiwemo majaji na mahakimu ili kuwajengea
uwezo utakaowasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao.
Akizungumza
na wanahabari leo jijini Dar es Salaam Jaji Rais wa Mahakama hiyo,
Nelson Kayobera amesema mafunzo hayo yatawsaidia kujua namna EACJ
inavyotekeleza majkumu yake pamoja na Sheria ya Mkataba wa Jumuia ya
Afrika Mashariki (EAC).
" Tumeanza mafunzo haya
tangu mwaka jana tumeanza na majaji na mahakimu wa mahakama keshokutwa
tutaenda Nairobi kuendesha semina hii," amesema Jaji Rais Kayobera.
Amebainisha
kuwa mahakama hiyo ina kesi zaidi ya 150 na kwamba ni jukumu la majaji
kujiua kwa kuisoma sheria za mahakama kwani zitawasaidia katika
utekelezaji wa majukumu yao.
Kwa upande wake,
Msajili wa EACJ, Yufnalis Okubo amesema mafunzo yamelenga majaji wa
mahakama hiyo kwani yatawasaidia kuijua sheria ya mahakama na kuisaidia
jamii kuzifahamu.
Nae Jaji wa Mahakama ya
Rufani ambaye pia ni Mkuu wa Chuo cha Mahakama- Lushoto, Dkt. Paul
Kihwelo amesema yatawahamasisha maafisa wa mahakama kuzitambua sheria
zake na kuelewa namna inavyotekeleza majukumu yake.
No comments:
Post a Comment