HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 26, 2022

Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki yatoa mafunzo kwa majaji na mahakimu

 


Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ) imetoa mafuzo kwa maafisa wa mahakama hiyo wa Tanzania wakiwemo majaji na mahakimu ili kuwajengea uwezo utakaowasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao.

Akizungumza na wanahabari  leo jijini Dar es Salaam Jaji Rais wa Mahakama hiyo, Nelson Kayobera amesema mafunzo hayo yatawsaidia kujua namna EACJ inavyotekeleza majkumu yake pamoja na Sheria ya Mkataba wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC).

" Tumeanza mafunzo haya tangu mwaka jana  tumeanza na majaji na mahakimu wa mahakama keshokutwa tutaenda Nairobi kuendesha semina hii," amesema Jaji Rais Kayobera.

Amebainisha kuwa mahakama hiyo ina kesi zaidi ya 150 na kwamba ni jukumu la majaji kujiua kwa kuisoma sheria za mahakama kwani zitawasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao.

Kwa upande wake, Msajili wa EACJ, Yufnalis Okubo amesema mafunzo yamelenga majaji wa mahakama hiyo kwani yatawasaidia kuijua sheria ya mahakama na kuisaidia jamii kuzifahamu.

Nae Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye pia ni Mkuu wa Chuo cha Mahakama- Lushoto, Dkt. Paul Kihwelo amesema yatawahamasisha maafisa wa mahakama kuzitambua sheria zake na kuelewa namna inavyotekeleza majukumu yake.  


No comments:

Post a Comment

Pages