January 05, 2022

Mahusiano ya Kidiplomasia Tanzania na Marekani yaimarika, yachochea maendeleo sekta ya afya, elimu, nishati na kilimo


Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (pichani) amesema uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Marekani ndani ya maka 60 umekua wa mafanikio makubwa kutokana na Taifa hilo linavyoisaidia Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, maji, nishati pamoja na miundombinu ya barabara  .


Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano wa kujadili Tathmini ya Miaka 60 ya Uhusiano wa Kidiplomasia kati ya Tanzania na Marekani uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere (JNICC).


Amesema kuwa nchi hiyo imekuwa bega kwa bega Tanzania kwani imetoa mchango mkubwa katika maeneo ya kisiasa na kiuchumi na kwamba katika kipindi hicho kumekuwa uwekezaji kwenye sekta ya afya na elimu.


Amebainisha kuwa  kwa miongo sita sasa Marekani imesimama na watu wa Tanzania katika kuwasaidia kufikia malengo ya maendeleo ya kitaifa kwa kuwawezesha katika nyanja mbalimbali.


Ameseistiza kuwa,  Marekani imekuwa ikisaidia maeneo ya kipaumbele yaliyobainishwa na viongozi wa Tanzania,ikiwemo Sekta ya Afya, umeme pamoja na Miundombinu ya barabara, ambapo Mataifa mengine yalikataa kuisaidia Tanzania.


"Katika kipindi changu cha uongozi  nilipomuelekeza Rais Barrack Obama kuhusu haja ya kuongeza upatikanaji wa umeme katika maeneo ya vijijini na kuinua tija katika kilimo kwa mara nyingine Marekani ilijibu kikamilifu"amesema Rais Mstaafu Kikwete.


Kwa upande wake, Balozi  wa Marekani Nchini Tanzania, Donald Wright  amefafanua kuwa anatarajia miaka 60 ijayo uhusiano wa taifa hilo na nchi ya Tanzania utazidi kuimarika zaidi kwa kuwasaidia hususani kwenye Sekta ya Afya lengo likiwa kupunguza vifo vitokanavyo na Ukimwi na mapambano dhidi ya Malaria.


"Marekani itaendelea kuwekeza katika eneo la afya ili kuhakikisha wanatokomeza janga la Ukimwi ambapo hadi sasa vifo vitokanavyo na ugonjwa huo vimepungua kwa asilimia 75 na kupambana na Malaria ili baada ya miaka michache kuweza kuitokomeza"amesema Balozi Donald.


Balozi Donald amesema Serikali ya Marekani inataka kuona Watanzania wanapata fursa ya kwenda kufanya  biashara hasahasa  kusafirisha bidhaa kwenda Marekani ikiwemo bidhaa za viwandani.


Nae, Mkurugenzi Mtendaji Taasisi inayojishughulisha na Utafiti wa Masuala ya Uchumi na Maendeleo (REPOA), Dkt. Donald Mmari amesema katika mkutano huo wamewashirikisha wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia cha Kurasini ili waweze kujua ni kwa namna gani mataifa hayo mawili yalivyoshrikiana katika kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia.


Pia amesema REPOA ipo miaka zaidi ya 25 na imekuwa ikifanya kazi kubwa kufanya tafiti zinazosaidia kupunguza tatizo la umaskini nchini kwa  


Ameongeza kuwa miaka 60 ya mahusiano hayo baina ya nchi hizo mbili yameleta manufaa makubwa ikiwemo kuimarisha usalama wa taifa la Tanzania na uwekezaji mkubwa kama miundombinu, afya na elimu na kufungua fursa kwa Watanzania kufanya biashara Marekani.


" Leo tumekutana hapa kujadili mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na Marekani, yameimarika sana, miaka 60 imezaa matunda makubwa katika maeneo ya kisiasa, kiusalama pamoja na kiuchumi"amesema Dkt. Mmari.

No comments:

Post a Comment

Pages