January 12, 2022

Mwenye 'degree' 9 kupambana na Dk.Tulia, Zungu, Sophia Simba kuwania nafasi ya Spika

* Walichukua fomu wafikia 17


AFISA Usimamizi wa Fedha Mkuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, mwenye degree 9, Prof. Handley Mafwenga akizubgumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Spika.


Na Asha Mwakyonde Dodoma

AFISA Usimamizi wa Fedha Mkuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, mwenye degree 9, Prof. Handley Mafwenga amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hivi karibuni aliyekuwa Spika wa Bunge hilo na Mbunge wa Jimbo la Kongwa Job Ndugai alijiiuzuli nafasi hiyo na kuwa wazi.

Baadhi ya wengine waliojitokeza kuwania nafasi ya Spika jijini Dodoma ni  Naibu Spika wa Bunge hilo Tulia Ackson, mbunge wa Mlimba Godwin Kunambi ambao walichukua fomu  jana, wengini ni Mussa Zungu, mbunge wa Tabora mijini Emmanuel Mwakasaka  ambao wamechukua leo.

Akizungumza jijini Dodoma leo Januari 11, 2022, mara baada ya kukabidhiwa fomu hiyo na Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Onganizetion Ccm Taifa, Solomon Itunda, Prof.Mafwenge  amesema kuna sababu zilizomsababisha kuchukua fomu hiyo.

Prof. Mafwenga amesema anaona kama mtumishi wa Umma  ushiriki wake utakuwa na tija katika Bunge kwa sababu tangu ofisi ya Spika ilivyoanzishwa chini ya ukoloni mwaka 1953 hadi linapatikana Bunge la Tanganyika baada ya uhuru mwaka 1961.

"Haijawahi kutokea mtumishi ambaye sio mbunge kwenda kugombea nafasi kubwa ya Spika kama hii. Nimelichambua Bunge na kulitathimini wengi wanafikiri ni Bunge la kisiasa hivyo nakanusha  katika utafiti wangu niliona Bunge ndio damu inayoendesha nchi lina sekta nyingi," ameongeza.

Huwezi kuwa na Bunge ambalo wanasiasa hawajui masuala ya viwanda na uchumi. Nina degree zaidi ya 9 zinazoshabiana na ueledi tofauti tofauti," ameeleza Prof. Mafwenga.

Amesema ana shahada ya juu ya LLB iliyojikita katika masuala ya kodi na kwamba amebobea katika masuala ya uchumi na pia anashahada ya uongozi aliyoipata kutoka nchini Uholand.

Prof. Mafwenga amesema kanuni ninataka zitafsiriwe hivyo hakuna haja ya kuwakatisha wabunge hoja zao endapo atapata nafasi hiyo atawaaikiliza hadi mwisho wakati wakitoa hoja.

Amesema wabunge wasitegemee kukutana na Spika ambaye hajui kitu endapo akipata nafasi watarajie zile kanuni zitatumika kiusahihi  hazita mkandamiza mtu zitatoa demokrasia  ili wazungumze chambuzi zao.

Prof. Mafwenga amesema wabunge watafurahi endapo atapata nafasi hiyo kwa kuwa anajua vitu vingi  hadi kwenye sekta ya michezo yupo vizuri.

Ameongeza kuwa  Bunge ni kitu ambacho kinaoanisha serikali ili watu wapate haki  na kwamba ni lazima Bunge hilo  liwe na ueledi hivyo  wabunge waende shule wakasome.

" Naijua Serikali kila sehemu kazi kubwa ya Bunge ni kutathimini  na kukagua kazi za Serikali na huwezi kuzikagua wakati huzijui," amesema

Ameeleza wabunge watambue  kwamba endapo atapata  nafasi ya  Spika watakuwa wamepata mtu sahihi lakini wakienda hovyo hovyo wataona wanabanwa demokrasia na wasijewakapiga kelele demokrasia hiyo inabana.

Prof. Mafwenga amesema lakini wabunge hao wakifanya vizuri watanenepa na wananchi wataona kuna uwakilishi mzuri bungeni.

No comments:

Post a Comment

Pages