Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda (kushoto), akimkabidhi nyaraka za ofisi ya Wizara ya kilimo, Waziri wa kilimo Hussein Bashe na pembeni ni Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde.
Na Asha Mwakyonde, Dodoma
WAZIRI wa Kilimo Hussein Bashe amesema kuwa mwaka kesho Wizara hiyo itatenga fedha kwa ajili ya kuwasomesha wataalamu katika vyoo bora vya kilimo.
Pia amemtaka Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Arolf Mkenda naye kutenga fedha lengo likiwa ni kupata wataalamu waliobobea kwenye masuala ya kilimo.
Kauli hiyo ameitoa jijini Dodoma jana wakati wa makabidhiano ya ofisi Bashe,alisema dunia imebadilika wanaweza kushuka katika masula ya kilimo wakidhani kinaendelea kwa mfumo ule ule wa miaka 60.
Bashe alisema wametoka Wizara ya Fedha na Mipango Mungu akijaalia kwa mara ya kwanza wizara kilimo inaweza kuwa na miradi mikubwa kwani kilimo ni biashara, Sayansi na kwamba wanaendelea kuwekeza katika sekta hiyo.
"Waziri wa Elimu kaka yangu Prof. Mkenda Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania ( COSTECH),ipo kwako lazima tuone ni namna gani unaweza kuiunganisha na Wizara ya kilimo,Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA), na vile vyuo vya kilimo 14," aliongeza.
Tutatenga bajeti kwa wanaoenda mafunzo ili 'field attachment' yao iwe kwenda kufanya kazi za Ofisa Ugani," alisema Waziri Bashe.
Alieleza kuwa wanafunzi wa chuo cha SUA wanaoenda mafunzo watatengewa bajeti kidogo ili baadae waende kufanya kazi za Ofisa Ugani katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Pia alisema kuwa wanafunzi hao watawakutanisha na ofisi ya Waziri mkuu ili wasaidiwe kujengewa uwezo kwa lengo la kubadilika maiaha yao.
Alisema kuwa atahakikisha mikakati ambayo waliweka na Waziri wa Elimu wakati wanafanya kazi pamoja ataiendeleza ipasavyo.
" Namshukuru Rais Samia Suluhu Hasaan kwa kuniamini na kuniteua katika Wizara ambayo nilishawahi kufanya kazi na tayani nina sehemu ya kuanzia hata niliposikia nimeteuliwa niliuliza naibu wangu ni nani. Nilifurahi nilipoambiwa ni Anthony Mavunde kwani kuna baadhi ya vitu alinishauri nikiwa katika Wizara hii," alisema.
Naye Waziri wa Elimu Prof. Mkenda alisema kuwa alichofurahi ni kukabidhi ofisi kwa mtu ambaye anaielewa vizuri Wizara ya kilimo.
Alisema kuwa walifanya kazi na Bashe na kwamba mafanikio mengi waliahirikiana na hata kwenye changamoto waliitana ofisini na kujadiliana.
"Tutafanya kazi pamoja wizara yangu haikwepeki tutakuwa pamoja," alisema Pro.Mkenda.
Aidha alimshukuru Rais kwa kumteua Bashe katika Wizara hiyo kwani ni mtu sahihi na anayeijua vizuri Wizara ya kilimo.
Wizara ya kilimo kutenga fedha za kuwasomesha wataalamu wake
Na Asha Mwakyonde,Dodoma

No comments:
Post a Comment