HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 20, 2022

SADA MKUYA: ANDIKENI HABARI ZENYE UBORA


 Waziri wa nchi afisi ya makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar Sada Mkuya Salum akimkabidhi Husna Muhammed wa Zanzibar leo Check ya Milioni moja na laki mbili baada ya kuibuka mshindi wa jumla katika tunzo ya kuandika habari za Tamwimu dhidi wanawake na uongozi Zanzibar.

 

Na Talib Ussi, Zanzibar

 

Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Dk. Sada Mkuya Salum amewakumbusha waandishi wa habari visiwani Zanzibar kuandika habari zenye ubora na Takwimu sahihi ili kuleta mabadiliko yaliokusudiwa.

 

Waziri Sada aliyaeleza hayo kwenye ukumbi wa Michenzani Moll katika tukio la kutoa tunzo kwa waandishi bora wa kuandika habari za Takwimu dhidi ya wanawake.

 

Alisema habari yoyote ambayo itaandikwa na kutumiwa takwimu sahihi ni rahisi kutoa muelekeo wa jamii au kundi fulani sehemu yoyote ile ya nchi.

 

Ukiandika kitu ambacho kina ushahidi ni tofauti na kuandika maneno tuu na takwimu huleta muelekeo na kuweka tahadhari nini kifanyike” alisema Dk.  Sada.

 

 Alieleza kuwa kama waandishi wa habari watajikita katika kuandika habari ambazo zitaonyesha uwiano wanawake na wanaume katika uongozi watakuwa wamesaidia kulinyanyua kundi la wanawake.

 

Alisema ili kuwe na usawa wa kijinsia kama inavyoelekezwa mikakati na mipango ya kitaifa na kimataifa, vyombo vya Habari vinapaswa kuweka uwiano sawa kati ya habari za wanawake na wananume.

 

Tunzo ya uandishi wa habri za Takwimu dhidi ya wanawake imeandaliwa kwa pamoja na chama cha wanahabari wanawake Tanzania (TAMWA) ofisi ya Zanzibar, chama cha wanasheria wanawake Zanzibar (ZAFELA) na PEGAO, kwa kujenga uelewa wa jamii juu ya usawa wa kijinsia.

 

Ambapo katika kupata mshindi wa tunzo hiyo zilichukuliwa kazi kwa mujibu vyombo kama ifuatavyo 73 zilikuwa za magazeti, tatu televisheni, 116 za redio na 260 za mitandao ya kijamii na kuwashukuru majaji wenzake kwa kufanya kazi hiyo kwa uadilifu na weledi.

 

Kwa mujibu wa  Mwenyekiti wa jopo la majaji wa tunzo hizo, Imane Duwe, alisema jumla ya kazi 452 kutoka katika vyombo vya Habari vya magazeti, redio, televisheni na mitandao ya kijamii ziliwasilishwa na kuchambuliwa.

 

Baada ya kazi kubwa ya majaji waliotangazwa kushida tunzo hiyo ni  Huwayda Nassor  kutoka Hits FM Redio na kujinyakulia kitita cha 1tsh. milioni, Haji Nassor Muhammed kutoka blog ya Pemba to Day pia alijinyakulia 1 milioni, Nusra Shaaban aliyeibuka mshindi katika habari za televisheni pia alipata kiasi kama hicho na Husna Muhammed wa Zanzibar leo yeye alikuwa mshindi wa ujumla na kuzawadia 1.2 milioni.

 

Mapema, Dk. Mzuri Issa Ali, ambaye ni Mkurugenzi wa  chama cha waanndishi wa habari wanawake Tanzania Upande wa Zanzibar  (TAMWA – Zanzibar)  alifahamisha  kuwa tuzo hizo zimebuniwa ili kuongeza umahiri katika uandishi wa Habari unaoshajihisha wanawake katika maswala ya uongozi.

 

Tunzo hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kuimarisha nafasi za wanawake katika uongozi (SWIL) unaotekelezwa kwa pamoja na ZAFELA na PEGAO kwa ufadhili wa Ubalozi wa Norway nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Pages