January 25, 2022

UDOM, Chuo Kikuu cha Nelson Mandela waanza utekelezaji meadi wa ujenzi wa maabara ya Akili Bandia

 

Na Jasmine Shamwepu, Dodoma

Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Nelson Mandela (Arusha) wameanza utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa maabara ya Akili Bandia (Robbot) kwa maendeleo ya africa (AI4D).
 

Sambamba na hilo Amesema kwa Tanzania itakuwa ni  watu wa pili kutengeneza  kwa teknolojia hiyo ya ujenzi wa  mradi maabara  ya Akili bandia (Robbot).


Kauli hiyo imetolewa  leo na Mohamed Hamid Abdallah katika uzinduzi wa mradi huo ambapo amesema kuanzishwa kwa teknolojia hiyo hakutoadhiri kwa shughuli za kazi za binadamu na ajira.


Kwa Upande wake mkuu wa chuo cha Nelson Mandela Profesa Emmanuel Luoga amesema Kamanda nchi tunaelekea uchumi wa kidigital hivyo eneo la tehama lazima litambulike ipasavyo ili kuleta mapinduzi katika viwanda na sekta zote.


Katika hatua nyingine amesema Kama nchi tunazoendelea ni wakati sasa wa kabadilika na haswa katika mitaala yetu na tulichukulie suala hili kama changamoto ili watoto wetu wote mashuleni wajue mambo ya tehama.


Kwa upande wake Msimamizi  wa mradi huo Ally  Njamawe amesema mradi una vigezo vitatu  utafiti,mafunzo na hatua ya tatu ni ubunifu ambao utakwenda kutatua changamoto katika sekta ya kilimo na afya ambapo kwenye sekta ya afya mgonjwa anaweze kupigwa X Ray na ikapelekwa kwenye kompyuta hiyo na kufanya kazi.


Aidha amesema wabunifu kumi katika sekta hizo ndio watakuwa wa kwanza kusoma masomo hayo ambapo kadri siku zinavyokwenda wataongeza wanafunzi wengine kwa ajili ya kujifunza zaidi.


Hata hivyo amesema ndani ya miezi sita watakuwa wamebobea katika tafiti na baada ya mwaka mmoja vyuo hivyo vitakuwa na kituo cha kuonyesha jamii.


Kwa upande wake mwanafunzi wa mwaka wa tatu chuoni hapo Innocent Charles amesema mradi huo utakwenda kuwasaidia wao kama wanafunzi .

No comments:

Post a Comment

Pages