January 25, 2022

Makinda: jamii msiwafiche watu wa makundi maalumu ndani wakati wa sensa


Spika Mstaafu wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda akizungumza na waandishi wa habari.

 

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

SPIKA Mstaafu wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda amesema  mwaka huu ni wa Sensa Kitaifa  jamii inatakiwa kutoa taarifa sahihi  ambayo zitaisaidia serikali kupanaga mipango yake.

Pia ameitaka jamii kutowafichi nyumabani watu wenye mahitaji maalumu na badala yake karahani wa Sensa watakapofika watoe taarifa za ukweli.

Haya aliyasema juzi katika mkutano wa Amani wa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania wenye lengo la kuipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha uchumi na kuendeleza miradi mikubwa ya maendeleo.

Makinda alisema faida ya sensa ni kubwa kuna watoto wengine wenye ulemavu, wazee, wenye matatizo wamefichwa nyumbani  hawajulikani.

" Huu ni mwaka wa Sensa itafanyika mwaka huu mwezi wa nane Rais Samia atatoa tarehe ya kuanza na itafanyika kwa kutumia vitongoji na mitaa," aliongeza.

Nawaomba wanajamii ya Maridhiano hili nalo mlisimamie watu wote wakaende kuhesabiwa," alisema Makinda.

Alisema lengo la kuhesabiwa ili serikali ijue ni watoto  wangapi wanaokwenda shule, Rais Samia amefanya jitihada za kujenga madarasa na mengine bado yanaendelea kujengwa.

Makinda alisema kuwa wanatakiwa kujua miaka 10 ijayo wale walioingia darasa la kwanza watakuwa chuo kikuu wapi ili serikali ijue kupanga kwa utaratibu isiwe ni suala la dharura.

Alisema itakapoanza watanzania wote wanatakiwa kuwa nyumabani karahani wa uabdikishaji zoezi la sensa watawakuta na kuwauliza maswali kwa ukarimu.

"Mtoe habari za kweli kusudi nchi ijipange huku kuna tatizo hili na huku kuna tatizo hili hata kama ni kuongeza hizo kodi tutafute maeneo mengine kama Zanzibar wanazungunzia uchumi wa bluu yote hayo ni kusaidia Watanzania," alisema.

Aliongeza kuwa ni suala la kisheria sio la hiari na pia ni la siri kwa wanafamilia.

No comments:

Post a Comment

Pages