January 14, 2022

Waliochukua fomu za kugombea Uspika wafikia 49


 Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Oganizetion ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa, Solomon Itunda kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Halmashauri kuu ya Taifa (NEC), CCM Itikadi na Uenezi  Shaka Hamdu Shaka akizungumza na waandishi wa habari.


Na Asha Mwakyonde, Dodoma


 KATIBU Msaidizi Mkuu Idara ya Oganizetion ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa, Solomon Itunda kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Halmashauri kuu ya Taifa (NEC),CCM Itikadi na Uenezi  Shaka Hamdu Shaka amesema kuwa hadi waliochukua fomu za kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wafikia 49.

Haya ameyasema jijini Dodoma  Januari 13,2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari katibu huyo amesa kuwa walichua fomu makao makuu ya Chama hicho ni wagombea 9, ofisi ndogo ya Dar es Salaam ni 10 na kwamba katika ofisi kuu kuu ya Zanzibar hakuna aliyechukua.

Aidha amewataka wanachama wa chama hicho kujitokeza kwenda kuchukua fomu hizo kwani ni haki yao ya kikatiba.

No comments:

Post a Comment

Pages