HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 16, 2022

Prof. Mkenda aweka jiwe la msingi ujenzi wa maabara ya TAEC


WAZIRI wa Elimu Sayansi  na Teknolojia  Profesa Adolf Mkenda akipata maelezo kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa maabara ya Tume ya Nguvu ya Atomiki Tanzania (TAEC).

 

 Na Asha Mwakyonde, Dodoma

WAZIRI wa Elimu Sayansi  na Teknolojia  Profesa Adolf Mkenda amesema kuwa serikali ina mkakati wa kuhakikisha vijana waliofanya vizuri katika masomo ya Sayansi wanapata ufadhili ( School ship) kwenda kuoma nje kwa lengo la kupata wataalamu wengi wa masula ya mionzi.

Pia amezitaka  Taasisi kutenga fedha Ili  kuwasomesha Wanafunzi bora wa sayansi wapate ufadhili na kwamba serikali inatarajia kuongea na walimu wanaofundisha nje ya nchi kuangalia namna ya kuweza kuwasaidia vijana wa kitanzanoa ambao wamejikitika katika masoma hayo.

Haya aliyasema jana jijini Dodoma wakati akiweka jiwe la msingi la maabara na Ofisi ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), alisema ili kuwe na Wanasayansi wa kutosha hapa nchini  na kuhakikisha vijana waliofanya vizuri kwenye masomo ya Sayansi wanapata ufadhili wa kusoma Vyuo vikuu nje ya Nchi.

Aliongeza kuwa kama serikali  Wanasayansi   na kwamba Wana  jukumu la kusomesha Watanzania  masuala. ya nguvu za Atomiki.

"Tukitenga fedha kila mwaka Watakuwa wanafunzi Bora wa masoma ya sayansi wakienda kusoma kwani Nchi nyingi zilizoendelea  ziliwekeza katika Sayansi tusidhani tuna uwezo wa kutosha," alisema Prof. Mkenda.

Prof  Mkenda alieleza kuwa  nchi inahitaji vijana wa kusoma Sayansi na Teknolojia Ili watumike na kwamba wanamkakati wa kuongea na balozi mbalimbali Ili vijana wanaofaulu vizuri masomo ya Sayansi wapate ufadhili.

" Taasisi zetu Chuo cha Teknolojia cha Dar es Salaam (DIT) na na Chuo cha Ufundi cha Arusha  wanatoa wabumifu wengi lakini tunawapeleka wapi ," alisema Prof. Mkenda.

Aidha waziri huyo amebainisha kuwa wanataka Shule zote ziingie kwenye Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), na Serikali itaanza taratibu kuwekeza kwenye Teknolojia na anaamini jambo hilo litasimama.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TAEC, Profesa Joseph Msambichaka alisema  wataanzisha ufadhili (schoolaship)  kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye Teknolojia ya nyuklia.

Alisema kuna mkakati wa kuanzisha Kiwanda cha Nyuklia nchini.ni.lazima kwenda sambamba na uwepo wa wataalam wa kutosha.

"Tunategemea kuanzisha mafunzo katika Sayansi ya nyuklia kwa kutumia wataalam waliopo TAEC na kuangaliwa kwa suala la kuondoa tozo ambazo si za lazima katika mionzi," alieleza.

Awali Mkurungenzi Mkuu wa TAEC, Profesa Lazaro Busagala alisema Serikali kupitia TAEC imeweka mikakati ya kusogeza huduma karibu na wananchi sawa na mpango wa watu wa maendeleo wa Taifa.
Alisema ujenzi huo mpaka kukamilika kwake utagharimu Sh bilioni 3.8  gharama hizo ni pamoja na kuweka mandhari nzuri na uzio.

Alisema jengo hilo litakuwa na Ofisi 27 chumba cha mkutano na maabara tano ikiwemo maabara za kupima sampuli ya vyakula na mazingira, maabara ya upimaji wa Viwango vya mionzi kea wafanyakazi, maabara ya matengenezo ya vifaa vya nyuklia, maabara ya sampuli mbalimbali za mazingira na maabara za ulinzi na usalama wa nyuklia.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya huduma za jamii Abdallah Chikota alisema kamati itaendelea kushirikiana na TAEC Ili wapate fedha za kutosha za kutekeleza majukumu yake.

TAEC ilianzishwa kwa sheria ya Bunge namba 7/2003, Awali ilijulikana kama Tume ya Taifa ya mionzi iliyoanzishwa na sheria ya Bunge namba 5 ya mwaka 1983.

Majukumu ya time hiyo ni kudhibiti matumizi ya mionzi Nchini kuhamasisha na kuendeleza matumizi salama ya Teknolojia na nyuklia  na kufanya Utafiti na kutoa ushauri na taarifa mbalimbali juu ya Sayansi, Teknolojia na nyuklia.

No comments:

Post a Comment

Pages