Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watu 3 wakiwa na
Vipande 25 vya Meno ya Tembo vyenye uzito wa Kg 20.9.
Akizungumza
jijini Dar es salaam Kamanda wa Kanda Maalumu ACP Jumanne Muliro
amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kufatia operasheni maalum ya kuzuia
uhalifu iliyofanyika kuanzia Feb 25 hadi Machi 9 mwaka huu.
Amebainisha
kuwa katika opareheni hiyo jeshi hilo kwa kushirikiana na limefanikiwa
Kikosi Kazi cha Kuzuia na kupambana Ujangili katika eneo la Ubungo NHC
Dar es salaam walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu wakiwa na
vipande 25 vya meno ya tembo vyenye uzito wa Kg 20.9.
Kamanda
Muliro alisema katika uchunguzi wa awali uliofanywa na jeshi hilo
umebaini meno hayo ni sawa na Tembo 14 walio uawa yalikutwa yakiwa
yamefichwa katika moja ya nyumba ya mtuhumiwa hao ambapo pia ilikutwa
gari yenye namba ya usajili T. 818 DCA Toyota Wiills iliyotumika
kusafirisha hayo.
Amewataja
watuhumiwa kuwa Gabriel Mgana, mkazi wa Ubungo NHC 2, Haffarman Yona
maarufu kama Mnyaturu mkazi wa Kinyerezi na Felician Cyril (57),
Mnyaturu mkazi wa Kinyerezi jijini Dar es salaam.
"Jeshi
la polisi linaendelea kufanya Uchunguzi wa kina kujua Tembo waliouawa
ni wa eneo lipi na thamani ya meno hayo ni kiasi gani na yalikuwa
yanatarajiwa kupelekwa au kuuzwa wapi" Amesema Kamanda Muliro.
Aidha
pia jeshi la Polisi katika operesheni hiyo pia limefanikiwa kuwakamata
Khatib Abdala Msambaab(33) mkazi wa Banana Kitunda, na wenzake 3 kwa
tuhuma za wizi kwa njia ya mtandao katika maeneo mbalimbali ya Jiji la
Dar es salaam.
Kamanda
Muliro amesema mara baada ya kukamatwa watuhumuwa hao ulifanyika
upekuzi wa kina katika nyumba za watuhumiwa hao na walikutwa na jumla ya
kadi (line) za simu 46 za kampuni tofauti tofauti, Vizibao 4 vya
uwakala
"Kumekuwepo
na matukio ya wizi kwa njia ya mtandao nchi katika oporasheni hiyo
watuhumiwa walikutwa na kadi (line) za simu 46 za makampuni mbalimbali
ambazo wamekuwa wakizitumia kufanyia uhalifu ikiwepo kujifanya wanatoa
huduma za kusajili kadi pamoja na huduma zingine ambazo utolewa na
makampuni ya simu" Amesema.
No comments:
Post a Comment