Na Mwandishi Wetu, Mihambwe
Afisa
Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu amezungumzia mwaka mmoja wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan madarakani kuwa
wenye mafanikio na wakijivunia mafanikio tele yaliyopatikana kwenye
nyanja mbalimbali za kielimu, afya, kichumi na kijamii.
Hayo
yamejili kwenye kikao kazi alichokifanya Gavana Shilatu kuzungumza na
viongozi ambapo amekiri Rais Samia kuupiga mwingi ndani ya mwaka mmoja
wake madarakani.
"Kwa
niaba ya Wananchi Tarafa ya Mihambwe tunajivunia mwaka mmoja wa Rais
Samia madarakani umejaa amani, utulivu, maendeleo na neema tele kwa
Tarafa ya Mihambwe. Mathalani Rais Samia ameleta Tsh. 500,000,000/-
kujenga kituo cha afya cha Tarafa ya Mihambwe; Rais Samia ameleta Tsh.
420,000,000/- kujenga Madarasa 21 shule za sekondari na msingi; Rais
Samia ameleta fedha kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo, fedha kwa
ajili ya kutoa huduma kwa jamii; Rais Samia ameendelea kuleta fedha
kutoa elimu bure. Kiukweli Rais Samia ameupiga mwingi sana kwetu wana
Tarafa ya Mihambwe na viunga vyake. Ahsante sana Rais Samia kwa
kutupenda Watanzania." Alisema Gavana Shilatu
Gavana
Shilatu pia aliwasisitiza viongozi kuwa wadau wazuri kueleza mambo
mazuri yaliyofanywa na Rais Samia kwa Wananchi kupitia mifano halisia ya
kimaendeleo iliyopo kwenye maeneo yao.
*Wakati
huo huo* Gavana Shilatu amefanya ziara kutembelea miradi mbalimbali ya
kimaendeleo ambapo amesisitiza uwazi, ushirikishwaji, ufanisi, kasi
kuikamilisha kwa wakati na ubora unaolingana na thamani ya fedha.
Katika
ziara hiyo Gavana Shilatu aliambatana na viongozi Serikali Kijiji,
viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliokuwa wakikagua utekelezaji
ilani ya uchaguzi CCM ambapo wameridhishwa na utekelezaji wake.
No comments:
Post a Comment