Tanzania Commercial Bank imeendelea na juhudi
zake za kuendelea kutanua huduma zake kwa kufungua matawi katika mikoa
mbalimbali hapa nchini ili kuhakikisha kila mtanzania anaitumia Tanzania
Commercial Bank.
Benki hiyo imetimiza haja yake hiyo kupitia huduma
zake mbalimbali katika kuigusa jamii kwa kufungua tawi jipya katika mkoa wa
Arusha wilaya ya Arumeru USA river katika hafla fupi iliyohudhuriwa na wadau
mbalimbali.
Tawi la USA River lilianzishwa mwaka 2007 kwenye
ofisi za posta, Usariver ikiwa ni benki ya kwanza kufika na kutoa huduma za
kifedha katika wilaya ya Arumeru Katika mkoa wa Arusha, Benki ya Biashara
Tanzania ina matawi sita (6) Arusha Meru,Usariver, Rombo, Mto mbu,Sokoine na
Tanzanite.
Tawi la Usariver lina jumla ya mawakala 60 ambao
wamesambaa katika wilaya ya Arumeru pamoja na kusogeza huduma za kibenki kwa
wananchi, Tanzania Commercial Bank pia inategemewa kufungua na kuendeleza fursa
mbalimbali za kibiashara kwa lengo la kuinua uchumi katika mkoa huo
Akiongea katika hafla ya uzinduzi wa Tawi hilo
Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank, Sabasaba Moshingi, alisema
wateja wa benki hiyo wapo katika mikono salama na kuwaomba wananchi waitumie
benki hiyo kwani imekuwa ikifanya mambo mengi yanayolenga jamii.
“Benki imepata mafanikio makubwa, kwa sasa Tawi
la Usariver lina jumla ya wateja 5,916 wanaofurahia huduma mbalimbali za
kibenki hususani mikopo yenye riba nafuu kama ya kilimo, biashara, watumishi na
wastaafu pamoja na kufanya miamala mbalimbali ya kifedha ndani na nje ya nchi.
Lakini vilevile, Tanzania Commercial Bank ni
wabunifu kwenye upande wa kidigitali tumeanzisha huduma ya kuweka akiba kwenye
vikundi ambayo tumeshirikiana naVodacom na tumeshakusanya zaidi ya Tshs bilioni
27 lakini pia sisi ni wamiliki wa huduma ya Songesha ni huduma inayomuwezesha
mteja kukamilisha miamala pale anapokua hanasalio.
Lakini kikubwa zaidi, Benki yetu imefanikiwa
kutoa kadi za Visa, hivyo basi wananchi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla
karibuni sana mjipatie Visa ATM card kwa kufanikisha miamala yeyote popote
mlipo Kwa kipindi cha mwaka 2020 mpaka February 2021 tawi limeweza kutoa mikopo
ya kiasi cha Tshs 5.78 Billioni kwa
wadau mbalimbali.
Kuna jumla
ya mawakala 60 wanaotoa huduma za kibenki katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa
Arusha. Kukua kwa biashara kumefanikisha benki kuhama kutoka katika ofisi ndogo
za TPC na kuhamia katika jengo Jipya tunalolizinduliwa leo lenye nafasi kubwa
na kuwezesha kutoa huduma kwa ubora na umahiri zaidi.
Kwa sasa
tawi lina wafanyakazi 12 waliobobea katika mambo ya fedha na benki wakitoa
huduma bora na kwa weledi wa hali juu.
“Benki yetu imekuwa mstari wa mbele katika
kusaidia maendeleo ya huduma za jamii; Tumefanikiwa kutoa misaada mbalimbali
ikiwa ni pamoja na kusaidia ujenzi wa bweni la Shule ya sekondari ya wasichana
Nduruma.”
Ni matarajio yetu kuwa biashara itaendelea kukua
na kutuwezesha kufungua matawi katika kila wilaya ili kuwezesha bidhaa na
huduma zetu kuwafikia watanzania wote kwa ukaribu zaidi .”
Benki imechangamkia fursa ya kukua katika wilaya
ya USA river, huku pia ikipanua uwepo wetu nchini.
Tawi linapatikana kwa urahisi, huduma zote za
kibenki zipo, pamoja na timu ya wataalam wenye ujuzi. Tunatazamia kukutana na
wakazi wa USA river, wafanya biashara na fursa zinazoifanya Benki ya Biashara
ya Tanzania kuwa mahali pazuri pa kufanya kazi.
Tanzania Commercial Bank pia inatoa huduma za
Kibenki Mtandaoni kama vile Internet Banking, Mobile App & Mobile Banking.
Lakini Benki pia iko karibu na wateja wake kupitia vituo vyetu vya Huduma kwa
Wateja.
Mkuu wa Mkoa Arusha, alitoa shukrani kwa Benki
kuweza kuwafikia wananchi wa Usariver na alitoa wito kwa wananchi ili kuweza
kuchangamkia fursa hususani makundi ya kina mama kwasababu Tanzania Commercial
Bank, ina akaunti maalum kwa ajili ya wanawake.
Aliongeza kwa kuishukuru Tanzania Commercial Bank
kwa kuendelea kuwekeza katika mkoa huo na kuwataka waendelee kuwekeza katika
wilaya zote za mkoa huo.
Mongella amewasisitiza wananchi wa Arusha wajitokezea kwa wingi kuchangamkia fursa zinazotolewa na Tanzania Commercial Bank kwani imekuwa benki ya kwanza kuwajali na kuwasogezea huduma wananchi wa mkoa huo.
No comments:
Post a Comment