HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 19, 2022

TFS BAGAMOYO YACHARUKA YANASA MAJAHAZI MAWILI YAKIWA YANATOROSHA MKAA KUELEKEA VISIWANI ZANZIBAR

 

Magunia ya mkaa zaidi ya 200 yakiwa katika moja ya jahazi ambayo yamekamatwa yakiwa yanasafirishwa kutoka wilayani Bagamoyo kuelekea katika visiwa vya Zanzibara kinyume na  taratibu za nchi.

 

Na Victor Masangu, Bagamoyo 

 

Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Bagamoyo wamefanikiwa kukamata zaidi ya magunia  200 ya mkaa ambayo yalikuwa yakisafirishwa kinyemela huku yakiwa yamepakiwa kwenye jahazi mbali kwa ajili ya kusafirishwa kwenda visiwani Zanzibar kiunyume kabisa na sheria na taratibu za nchi.

 

Akizungumza mara baada ya kukamata magunia hayo Afisa misitu msaidizi wa Tfs daraja la pili kutoka Bagamoyo  Mohamed Saimon alibainisha kwamba watahakikisha wanaendelea kufanya misako katika sehemu zote lengo ikiwa ni kuwabaini wale wote ambao wanavuna mazao ya misitu bila kuzingatia sheria pamoja na kukwepo kulipa kodi ya serikali.

 

“Tumefanikiwa kukamata majahazi mawili ambayo yalikuwa yamepakia zaidi ya magunia yapatayo 200 ambayo yalikuwa yanasafirishwa kinyume kabisa na sheria za nchi na yalikuwa yanapelekwa visiwani Zanzibar kinyume kabisa na taratibu za mazao na misitu na kwamba lengo letu ni kutunza mazingira na sio kuharibu misitu ya asili,”alisema Saimon

 

Aidha alifafanua kuwa katika kukabiliana na wimbi hili la ukataji wa miti ovyo wataendelea na zoezi la kuwasaka wale wote ambao wanajihusisha na biashara hiyo ili waweze kukwamatwa kwani wanasababisha serikali kukosa mapato kutokana na kukwepa kulipa kodi.

 

Kwa upande wake mhifadhi wa TFS kanda maalumu ya saadani na Bagamoyo amesema kwamba serikali inaendelea kufanya jitihada ili kuhakikisha inadhibiti wimbi la  ukataji wa miti ovyo pamoja na kuweka ulinzi madhubuti ambao utasaidia katika utoroshwaji wa rasilimali misitu na pia watahakikisha wanaendelea kuitunza na kuilinda.

 

Naye Mkuu wa Wilaya  ya Bagamoyo amekemea na kulaani vikali vitendo hivyo vya kufanya magendo katika misuti na kwamba kwamba serikali haitawafumbia macho wale wote ambao watahusika na biashara hiyo ya kufanya uharibifu mkubwa wa mazingira na kuwataka wananchi wote kuachana kabisa mara moja vitendo hivyo na watafanya msako mkali katika bandari zote  ambazo ni bubu.

 

 “Sisi kama serikali ya Wilaya yetu ya Bgamoyo hatuwezi kufumbia macho kabisa suala hili la biashara za magengo na tutahakikisha vitendo hivyo vyote tunavikomesha kabisa na pia tutafanya oparesheni mbali mbali katika bandari zote bubu ili kuweza kudhibiti hali hii ambayo inafanywa na baadhi ya watu kutuharibia misitu yetu,”alisema Zainab,

 

Katika hatua nyingine aliwawataka watendaji wa vijiji na viongozi mbali mbali kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo ikiwa sambamba na kuwabaini na kuwafichua wale wote ambao wanahusika na uharibifu huo wa kukata miti na kuendesha biashara za magendo kinyume kabisa na sheria na taratibu za nchi na kwamba ameahidu kulivalia njuga suala hilo.

No comments:

Post a Comment

Pages