April 25, 2022

*KINANA AWATAKA WABUNGE NA MADIWANI KUTOPITISHA SHERIA ZINAZOMINYA HAKI NA KUWABANA WANANCHI

 

 
Balozi wa zaidi ya miaka 25 katika tarafa ya Korogwe Mjini Mika Mwirongo  akifurahi kumuona Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Abdulrahman Kinana kwenye mkutano uliyofanyika katika ukumbi wa Lembeni mjini Korogwe.



Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amewataka  madiwani na wabunge kukataa  kupitisha  miswada ya Sheria  yenye kukandamiza haki na kuminya fursa ya wananchi wanyonge kujiendeleza kiuchumi.

Pia, amesema Sasa ni wakati muafaka  kulitazama vyema  kundi la wajasiriamali wadogo wakiwemo mamalishe na bodaboda ili wawekewe mazingira mazuri ya kunufaika na juhudi zao.

Kinana ameyasema hayo leo mjini Korogwe, wakati akizungumza na wana CCM katika ukumbi wa Lembeni, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na kujitambulisha kwa wanachama.

"Madiwani nyinyi ndio mnaosimamia sheria za Halmashauri, mkiona sheria hazina uhusiano na wananchi kataeni. Mkiletewa sheria pelekeni kwa wananchi waulizeni, rahisisheni maisha ya watu muwasidie wakue.

"Wabunge wa Bungee la Jamhuri ya Muungano...sheria ikija bungeni waambieni (serikali) kwa sasa hatuipitishi mpaka tukashauriane  na wananchi," alisema.


No comments:

Post a Comment

Pages