HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 28, 2022

Mradi wa #NGO Kidijitali kwa mashirika yasiyo ya Kiserikali wazinduliwa Tanzania


Mkurugenzi wa Taasisi ya Media Convergency, Asha Abinallah, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa #DigitalNGO ambao unatarajiwa kuwa kichocheo cha mabadiliko na mapokeo ya kidijitali kwa mashirika yasiyo ya kiserikali nchini Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano na kutoka Wizara ya Habari, Mulembwa Munaku, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa #DigitalNGO ambao unatarajiwa kuwa kichocheo cha mabadiliko.
Mwakilishi kutoka META, Desmond Mushi.
Msajili wa Mashiriki yasiyokuwa ya kiserikali, Vickness Mayao, akizungumza katika uzinduzi huo.
 
 
Dar es Salaam, Tanzania

Media Convergency kwa kushirikiana na Meta imetangaza mfululizo wa programu za ujenzi wa mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo ni muendelezo wa programu ya majaribio ambayo ilianza katika H2 2021. 

Programu za Meta za mashirika yasiyo ya kiserikali pia zimetekelezwa nchini Nigeria na Afrika Kusini
kupitia mfululizo wa ushiriki ikiwa ni pamoja na mafunzo, vikao vya kusikiliza na warsha kwa mashirika yasiyo ya kiserikali. 
 
Malengo makuu ni katika kujenga thamani katika jamii, kuungana na washirika zaidi  na kuhakikisha majukwaa yao yanatumiwa kama nguvu ya matokeo bora. Meta inalenga kusaidia sekta  ya mashirika yasiyo ya kiserikali na ambayo yamekuwa washirika katika kuleta matokeo chanya kijamii  katika ukanda wa kusini mwa jangwa la Sahara, kujifunza kuongeza matokeo chanya katika kazi zao  kupitia matumizi ya majukwaa ya Meta na kutumia teknolojia za kidijitali.

Lengo la mradi wa #NGOYAKIDIJITALI ni kushawishi mabadiliko ya kidijitali kupitia njia sahihi, ili
kuhamasisha mazungumzo na hatua za ukamilifu wa kuhamia kidijitali kwa kutumia zana za kiteknolojia
kwa jamii ya mashirika yasiyo ya kiserikali nchini Tanzania. 
 
 
Malengo haya yanaungwa mkono na
dhamira ya Meta kwa ukuaji wa Tanzania, kwa kutekeleza mipango inayosaidia mashirika yasiyo ya
kiserikali na sekta ambazo zimekuwa na mchango chanya kwa jamii nchini kwa nia ya kujenga
ushirikiano wa kimkakati na washirika wa ndani na wadau wa sera katika nafasi ya maendeleo ya kijamii. 

Mradi huo utazingatia kutumia mpango wa Uangalizi awali (Incubation) wa miezi sita ambayo italenga
mashirika yasiyo ya kiserikali yapatayo 35 na mpango maalumu wa mafunzo kwa mashirika hayo
(Ujenzi wa uwezo wa dijiti) kwa watu wapatao 1,000 katika miezi kumi na miwili ijayo, pamoja na
ushirikiano na wadau muhimu wa kimkakati kuelekea utekelezaji wa ajenda hii na mgawanyo wa
rasilimali katika hali ya mazingira ya kidijitali kwa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkurugenzi wa Sera ya Umma katika ukanda wa Afrika Mashariki, Mercy Ndegwa alisema "Katika Facebook, lengo letu ni kuwapa watu uwezo wa kujenga jamii na kuileta dunia karibu zaidi. 
 
Tunatambua  kwamba mashirika yasiyo ya kiserikali yanajukumu muhimu katika jamii na ni sehemu muhimu ya jamii yetu, na hivyo kuwa sehemu muhimu ya mradi huu.
 
 Hii ndiyo sababu tunafurahi kuanzisha programu hizi nchini Tanzania ili kuwapa mashirika yasiyo ya kiserikali zana wanazohitaji ili kuongeza matokeo katika kazi zao. 
 
Tunalenga kuharakisha uwezo wa sekta ya kijamii katika kuendesha mabadiliko ya kijamii  yenye tija, manufaa na tunatafuta kufikia lengo hili miongoni mwa mashirika yasiyo ya kiserikali nchini  Tanzania."

Asha Abinallah, Mkurugenzi Mtendaji, Media Convergency Tanzania alisema "kazi yetu ya kuhamasisha  Mabadiliko ya Kidijitali imejengwa kwa msingi wa maslahi ya kweli katika kuelewa na kusaidia  ushirikiano wa mashirika yasiyo ya ya kiserikali kuhusiana na teknolojia zinazojitokeza na kutumika.
 
 Hii  pia inajenga juu ya ripoti; "Muhtasari wa jumla wa Ekolojia ya kidijitali, Matumizi ya teknolojia ibukizi kwa mashirika yasiyo ya kiserikali nchini Tanzania” iliyozinduliwa na Media Convergency mwaka 2021. 

Tangu ripoti ilivyozinduliwa, Mashirika yasiyo ya kiserikali yapatayo thelathini na saba (37)
yamefundishwa kupitia mpango wa mafunzo ya majaribio katika H2 2021 na tunatarajia kufikia mashirika yasiyo ya kiserikali mengi zaidi kupitia ushirikiano wetu na Meta. 

Tunajiwasilisha kwa unyenyekevu kwa jamii ya mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau wengine
wanaohusika nayo kwa namna moja au nyingine na tunaahidi kuwa tutato huduma thabiti kwa kadiri ya
ujuzi na uwezo wetu. Kwa pamoja tunaweza kuipeleka Tanzania katika uchumi wa kidijiti uliokomaa katika mapinduzi haya ya nne ya viwanda.

No comments:

Post a Comment

Pages