HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 13, 2022

TCB KUENDELEA KUWA MDAU WA MAENDELEO KATIKA KUBORESHA UCHUMI WA TANZANIA

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Makame Mbalawa  akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank, Nd Sabasaba Moshingi  alipotembelea banda laBenkihiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa reli ya kisasa kipande cha nne (SGR) kinachotoka Tabora hadi Makutupora, Mkoani Dodoma iliyofanyika Cheyo B, Mkoani Tabora.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Makame Mbalawa  akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank, Nd Sabasaba Moshingi (kulia), wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa reli ya kisasa kipande cha nne (SGR) kinachotoka Tabora hadi Makutupora, Mkoani Dodoma iliyofanyika Cheyo B, Mkoani Tabora.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank, Nd Sabasaba Moshingi  akiweka udongo kwenye jiwe la msingi wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa reli ya kisasa kipande cha nne (SGR) kinachotoka Tabora hadi Makutupora, Mkoani Dodoma iliyofanyika Cheyo B, Mkoani Tabora leo ambapo katika uzinduzi huo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Makame Mbalawa akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanian Mh Samia Suluhu.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank, Nd Sabasaba Moshingi akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa reli ya kisasa kipande cha nne (SGR) kinachotoka Tabora hadi Makutupora, Mkoani Dodoma iliyofanyika Cheyo B, Mkoani Tabora.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Makame Mbalawa akiwa katikapicha ya pamojana wakuu wa idara kutoka taasisi mbalimbali


Tanzania Commercial Bank TCB) imesema itaendelea kuwa mdau mkubwa wa maendeleo  ili kuboresha uchumi wa Tanzania.


TCB imeshirikia kikamilifu katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha kutoka Tabora mpaka Makutupora Mkoani Dodoma.

Hayo yamesemwa na Afisa  Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi  wakati wa uzinduzi wa mradi wa uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa reli ya Kisasa (SGR) awamu ya nne leo Mkoani Tabora

Moshingi amesema, Tanzania Commercial Bank  ni benki kubwa nchini  na  wamejitoa na wameshiriki kwa hatua kubwa katika kuhakikisha shirika la Reli Tanzania (TRC) linafanikisha mradi wa SGR Lot 3 kwa mafanikio makubwa.

“Tanzania Commercial Bank ni wadau wakubwa wa maendeleo hapa nchini na kuchangia ujenzi wa Taifa, TRC ni wenzetu hivyo mradi huu wa SGR utaleta mafanikio kwa mkoa wa Tabora,”amesema

“Kufanikiwa kwa mradi huu kutarahisha usafiri wa kutoka Tabora hadi Dar es Salaam kwa masaa sita, na treni ya mizigo kwa masaa kumi pia kutafungua fursa za kiuchumi kwa mikoa ya Tabora, Dodoma, Singida , Shinyanga hadi Mwanza,”amesema

Moshingi amesema, wananchi wa Tabora kwa sasa wataanza kukua kiuchumi, kwa kusafirisha mazao yao kwenda Dar es Salaam ambapo ndio soko kuu la biashara na usafiri utakuwani ni wa uhakika zaidi.

Amewahisi wakazi wa Tabora kujipatia huduma Bora zinazopatika Tanzania Commercial Bank ili waweze kwenda na kazi ya Uchumi kupitia mradi huo "amesema

Moshingi ameeleza kuwa kwa Sasa Tanzania Commercial Bank ina matawi kila pembe ya Tanzania hivyo imejipanga vema kutoa huduma kwa watanzania pamoja na wageni kutoka nje.

No comments:

Post a Comment

Pages