Naibu Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe akifungua Warsha hiyo.
Kiongozi wa Mradi huo wa TRADE HUB nchini Tanzania Prof. Reuben
Kadigi akizungumza na wadau lengo la warsha hiyo.
Mhadhiri Muandamizi wa Uchumi Kilimo na Masoko Dk. Fulgence Mishili akitoa salamu kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo.
1. Mtafiti kutoka SUA Dk. Charles Mgeni akizungumza neno la shukrani kwa mgeni rasmi kwaniaba ya Rasi wa Ndaki ya Uchumi na Stadi za Biashara Kilimo.Joseph Kangile Mtafiti wa Mazao ya Kahawa, Sukari na Soya akitoa wasilisho kwa wadau kusuhu matokeo ya awali katika zao la kahawa.
Wadau waliojitokeza wakifatilia mawasilisho tofauti
tofauti.
Mawasilisho yakitolewa.
Wadau wakifatilia mawasilisho tofauti tofauti.
Amina Hezron na Calvin Gwabara, Dodoma.
SERIKALI kupitia Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara
imekipongeza na kukishukuru Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwanamna
ambavyo kinafanya tafiti ambazo zinalenga kuinua maendeleo ya Watanzania kwakufungamanisha
maswala mbalimbali yanayolenga kuboresha uchumi na kuleta maendeleo kwa
taifa.
Akizungumza kwenye warsha ya wadau wa mradi wa Biashara
Maendeleo na Mazingira Naibu Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara mhe. Exaud
Kigahe amesema kuwa mradi huo unatekelezwa katika kipindi muafaka ambacho
serikali inasisitiza uwekezaji kupitia sera ya nchi ya kuinua uchumi kupitia
uwekezaji katika sekta ya viwanda na biashara.
“Imani yangu kuwa kwakipindi hiki cha miaka mitano ambayo mradi
huu utatekelezwa utasaidia sana kufungamanisha shughuri za biashara za bidhaa
za kilimo Wanyama pori na sekta nyingine ili kuhakikisha kuwa biashara ya mazao
haya yanakuwa kichocheo chaukuaji wa uchumi ambao tunasema uwe shirikishi ili
kupunguza umaskini na kuleta maendeleo endelevu”, alisema Mhe Kigahe.
Akizungumzia dhumuni la warsha hiyo Kiongozi wa Mradi wa huo wa
TRADE HUB nchini Tanzania Prof. Reuben Kadigi amesema kuwa ni kuwasilisha
matokeo ya awali ya utafiti wa mradi huo wa kile ambacho kimeshapatikana kwa
muda mfupi kwa utafiti wa awali .
“Mradi unatafiti athari za biashara kwa ulimwengu na watu
gharama na manufaa tutumie rasilimali tulizonazo kuleta maendeleo ambapo
tukitumia bila mpangilio mzuri inawezekana uwendelevu usiwepo tutakuwa
tumeharibu uhalisia” alisema Prof. Kadigi.
Prof. Kadigi ameeleza kuwa mradi huo unatekelezwa ili kusaidia
kubaini suluhu za kupunguza athari hasi na kuimarisha manufaa sawa kuweza
kuweka bayana hatari za biashara zinazotokana na desturi au vitendo vya
kimazoea ambavyo si endelevu kijamii na kimazingira pia .
“Jukumu letu kama mradi kushughurikia changamoto ngumu ya jinsi
ya kuondoa athari mbaya kwa jamii na mazingira zinazosababishwa na biashara
tufanye biashara ambayo itatusaidia kutuendeleza kuleta maendeleo lakini pia
kuzingatia madhara kwenye uhalisia wa mazingira “, alisema Prof Kadigi.
Prof. Kadigi amesema lengo la mradi huo ni
kuhakikisha biashara ya mazao ya kilimo na Wanyamapori inakuwa chachu ya ukuaji
wa uchumi shirikishi kupunguza umasikini na moja ya njia ya utekelezaji wa
maendeleo endelevu kama inavyotajwa na Maendeleo Endelevu bila kuchangia zaidi
uharibifu wa mazingira na upotevu wa viumbe hai huku ukiwa umelenga kufanyia
katika sekta ndogo za Sukari,Soya Kahawa, Nyama pori na Wanyamapori.
Kiongozi wa Mradi amesema mradi huo ni wa miaka mitano
umeanza mwaka 2019 na utakamilika mwezi machi Mwaka 2024 na unatekelezwa na
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwakushirikiana na washirika kutoka nchi
15 tofauti za Afrika, Asia Uingereza na Brazil.
Akizungumza kwaniaba ya Makamu Mkuu wa Chuo Mhadhiri Muandamizi
wa Uchumi Kilimo na Masoko Dk.Fulgence Mishili amesema Chuo kikuu cha Sokoine
kitaendelea kuhakikisha kitafanya tafiti na kutoa huduma za ushauri wa
kitaalamu kwa jamii na taifa ili kuiwezesha serikali kufanya maamuzi sahihi
kupitia matokeo ya tafiti za kisayansi.
Amewashukuru wadau wote waliojitokeza katika warsha hiyo
kwakutenga muda na kushiriki katika tukio hilo muhimu na kuwataka kusikiliza
kwa makini matoke ohayo ya awali ya tafiti tano zilizofanywa na waweke
mapendekezo na ushauri wa kina kama kuna mambo ambayo yamesahaulika kwenye
matoke ohayo ya awali.
Akizungumza kwaniaba ya Rasi wa Ndaki ya Uchumi na Stadi za
Biashara Kilimo Mtafiti kutoka SUA Dk. Charles Mgeni ametoa shukrani kwa Mhe.
Kihage kwa hotuba ambayo amesheheni nasaha zenye kujenga na kuleta matumaini
katika juhudi za kuwafikisha kuwa biashara na bidhaa za mazao ya kilimo pamoja
na wanyamapori inakuwa engine ya ukuaji jumuishi wa kiuchumi na kupunguza
umasikini.
“Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kitanendelea kushirikiana na
serikali kutafuta ufumbuzi na kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili
biashara ya bidhaa ya kilimo pamoja na ya wanayamapori hapa nchini lengo
ni kuboresha sera za kibiashara na uchumi ili kuleta tija na ufanisi kwa wananchi
wetu wanaojishughulisha na shughuri hizi”, alisema Dk. Mgeni.
No comments:
Post a Comment